Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge akimkaribisha mgeni Rasmi ili aweze kuzindua maadhimisho ya wiki ya Mazingira duniani katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu akitoa maelezo kwa mgeni Rasmi Mheshimiwa Samuel Sitta alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais katika maadhimisho ya wiki ya siku ya mazingira jijini Tanga. Wengine wanaosikiliza ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt Binilith Mahenge (kulia) na Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (kulia).
Watanzana wametakiwa kutunza na kuthamini mazingira kwa sababu ni urithi wa thamani kubwa sana kwa kizazi cha sasa na kijacho. Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya siku ya mazingira Duniani, Mheshimiwa Samuel Sita- Waziri wa Uchukuzi ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Mohammed Gharib Bilal.
Akiongea na Wananchi katika viwanja vya Tangamano vilivyopo katika jiji la Tanga Mheshimiwa Sita amesisitiza juhudi zaidi katika suala zima la utunzaji wa mazingira na kuwaomba Wazazi kuelemisha watoto wao umuhimu wa kuthamini mazingira. Aidha amewapa hongera Wananchi na Viongozi wa jiji la Tanga kwa kutilia mkazo usafi wa mazingira na kufanya jiji hilo kuibuka mshindi wa tatu katika mashindano ya usafi wa mazingira kitaifa.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi ili kufungua sherehe hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Binilith Mahenge aliesma ni jukumu la kila mmoja kutunza na kuhifadhi mazingira hivyo basi kila Mwananchi ajitahidi katika hilo.
Siku ya mazingira duniani hufanyika kila tarehe tano ya mwezi Juni kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Ndoto bilioni saba, dunia Moja , tumia Rasilimali kwa uangalifu. Hii ikimaanisha kutumia vema rasilimali zetu ili kutunza vema mazingira yetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...