Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya dola Bilioni 30 kwa ajili ya Kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini. Hafla ya kutiliana saini ilifanyika jana, Seronela mkoani Arusha ambapo waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress walisaini makubaliano ya dola 2milioni kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya ujangili n anyingine milioni 14.5 kwa ajili ya uhifadhi. 
 Balozi huyo wa Marekani Mark Childress, alimwelezea Nyalandu, kuwa ni mwanasiasa jasiri na makini asiyeogopa kusema ukweli hata kama unaumiza. Balozi Childress amesema waziri huyo ni tofauti na wanasiasa wengine na kwamba, ujasiri wake katika utendaji unapaswa kuungwa mkono. Kauli ya Balozi huyo imetokana na uamuzi wa Nyalandu kuweka hadharani idadi ya tembo waliopo nchini na kueleza bayana kuwa, tatizo hilo bado ni janga kwa taifa. 
“Kwa mwanasiasa mwingine ingekuwa ngumu kutoa taarifa kama ile kwani angeona anajimaliza lakini alilazimika kufanya hivyo ili njia za kutokomeza tatizo hilo ipatikane na sasa marafiki wa uhifadhi tumeamua tupambane pamoja kulaliza tatizo hili”. 
Pia, katika taarifa yake Nyalandu hakusita kueleza kutoweka kwa tembo 10,000 ambao hawakuweza kuonekana wakati wa sensa ya mwaka 2014 iliyofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa. Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano na uzinduzi wa mradi mkubwa wa kulinda mazingira, kukuza uhifadhi na utalii nchini wa PROJECT, ambapo serikali ya Marekani imetoa zaidi ya sh. Bilioni 31 katika utekelezaji wa mradi huo. 
Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Treetops iliyopo ndani ya eneo la Hifadhi ya Wanyamapori inayosimamiwa na jamii (WMA) kwenye Hifadhi ya Taifa ya Tarangire. 
 Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na balozi wa Marekani, Mark Childress wakisaini mktaba wa kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini jana, Tarangire mkoani Arusha ambapo serikali ya Marekani imetoa dola milioni 14.5 na dola 2milioni kwa ajili ya vita dhidi ya ujangili(Sh20bilioni) kwa ajili hiyo. mapambano dhidi ya ujangili
 Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na balozi wa Marekani, Mark Childress wakioingezana baada ya  hati za mkataba wa kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini jana, Tarangire mkoani Arusha ambapo serikali ya Marekani imetoa dola milioni 14.5 na dola 2milioni kwa ajili ya vita dhidi ya ujangili(Sh20bilioni) kwa ajili hiyo. mapambano dhidi ya ujangili
Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na balozi wa Marekani, Mark Childress wakibadilishana hati za mkataba wa kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini jana, Tarangire mkoani Arusha ambapo serikali ya Marekani imetoa dola milioni 14.5 na dola 2milioni kwa ajili ya vita dhidi ya ujangili(Sh20bilioni) kwa ajili hiyo. mapambano dhidi ya ujangili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2015

    Vivution vya utalii vingi tu, Tanga tungekua na utalii, Mtwara nako utalii undekuwepo, Selous ingekuwa nchi nyingine huko na utalii ungekuwa juu sana, raslimali tunazo kazi kwetu kuziendeleza, msaada huu uelekezwe huko.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2015

    Ujangili unatumalizia fursa tusiruhusu ukite mizizi. Wenyeji wanaoishi kwenye maeneo yanayozingira mbuga za wanyama washirikishwe na kuhamasishwa katika kufichua na kupiga vitaa ujangili. Hii ni kwa faida yetu wenyewe na mustakabali wa uchumi wetu wa sasa na baadaye.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2015

    dolla billioni 30 ni pesa nyingi sana kuliko hata bajeti ya wizara

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2015

    Tatizo kubwa moja ni kuwa serikali ndio inayotuchanganya watu wa Tanzania. Upande mmoja inapokea misaada ya kuimalisha utalii wakati huohuo upande mwingine inaingiza wachina wasio na shughuli maalum nchi kwa wingi hali taarifa tulizonazo mpaka sasa ni kuwa wachina wanahusika kwa asilimia 100 ktk mauaji ya tembo wengi nchini na wizi wa nyara za nchi kama wanyama, ndege na viumbe wengine wengi wa mwituni na baharini. Marekani ingesimamia miradi hiyo yenyewe pesa hizo hazitafikia mahitaji halisi ya sekta. Serikali hii dhalimu imeshindwa ktk mengi sana hakuna mfano mpaka sasa! Nyerere hakukosea kumkataa rais huyu mwaka 1995! Matendo yake ktk miaka 10 ya utawala wake wa rushwa iliyokithiri, udini mkali, mporomoko wa maadili ya utumishi wa umma, matumizi mabaya ya dola hasa mahakama bunge na polisi na upendeleo wa kidugu na kirafiki ktk kutoa kazi na zabuni za serikali. Natamani aishi muda mrefu ili aone aibu yake siku moja!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...