Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akilakiwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vijana, waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani Ruvuma kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000. Picha zote na John Badi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwapungua mkono wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi, waliofurika nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, fomu zilizotiwa saini na wanachama wa CCM mkoani humo, waliofika kwenye Ofisi hizo jana, kwa ajili ya kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...