Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati) akionyesha kabrasha lenye fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kushoto ni Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa (Nec) ya CCM wa Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu. Kulia ni mkewe Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lihamba. Tukio hilo la uchukuaji wa fomu lilifanya katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akiwaonyesha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabrasha lenye fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kabla ya kuanza kuzungumza na kujibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari. Kulia ni mkewe Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lihamba. Tukio hilo la uchukuaji wa fomu lilifanya katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Waziri Chikawe ambaye alijibu maswali ya waandishi wa habari kiufasaha huku akishangiliwa na wanachama hao, alisema yeye ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa na pia akiteuliwa na chama chake kugombea nafasi hiyo ataendeleza mapambana zaidi dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini pamoja na adui mwingine rushwa ambaye ni adui wa maendeleo. Kulia ni mkewe, Profesa Amandina Lihamba.
Huyu si ndiye waziri wa mapolisi, kwa hiyo tutapigwa mpaka tukome. Kweli urais nchini kwetu ni usanii, kila mtu anaona anafaa ndiyo maana kuna msururu wa watu wanaofikiria wanafaa.
ReplyDeletesas hii kugombea URAIS imekuwa kama kuomba kuingia chooni kila mtu ana subiri zamu yake na yeye aingie,ukiona makada wa chama chochote cha siasa wana kimbilia ikulu ujue wamechoka kazi wanatafuta kupumzika bila gharama, pia ni dalili za kuwa chama husika hakina mwenyewe tena watoto wazee vijana wote wana pigana vikumbo kugombea uongozi wa chama ujue nidhamu na maadili sio kigezo tena nawaombea mwisho mwema wote.
ReplyDeletemdau.
Dodoma.
Anony acha zako bana, polisi kwa tz ni rafiki tu.
ReplyDeleteWacha wagombee kama wanaona wanaweza wameona kizungu wanakijua, kuongiza wananchi na kuongea na mataifa mengine wanaweza kwa nini wasijitoe wacha waombe kazi. Sijui kama Kamati kuu ina kompyuta ya kutema wale wasiokuwa na vigezo vinavyotakiwa, kabla haijaingia kwenye usaili.
ReplyDeleteHawa ndio viongozi tunataka kumrithi JK hakuna longolongo kazi tu. Hongera waziri chikawe
ReplyDelete