Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati) akionyesha kabrasha lenye fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kushoto ni Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa (Nec) ya CCM wa Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu. Kulia ni mkewe Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lihamba. Tukio hilo la uchukuaji wa fomu lilifanya katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akiwaonyesha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabrasha lenye fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kabla ya kuanza kuzungumza na kujibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari. Kulia ni mkewe Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lihamba. Tukio hilo la uchukuaji wa fomu lilifanya katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Waziri Chikawe ambaye alijibu maswali ya waandishi wa habari kiufasaha huku akishangiliwa na wanachama hao, alisema yeye ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa na pia akiteuliwa na chama chake kugombea nafasi hiyo ataendeleza mapambana zaidi dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini pamoja na adui mwingine rushwa ambaye ni adui wa maendeleo. Kulia ni mkewe, Profesa Amandina Lihamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2015

    Huyu si ndiye waziri wa mapolisi, kwa hiyo tutapigwa mpaka tukome. Kweli urais nchini kwetu ni usanii, kila mtu anaona anafaa ndiyo maana kuna msururu wa watu wanaofikiria wanafaa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2015

    sas hii kugombea URAIS imekuwa kama kuomba kuingia chooni kila mtu ana subiri zamu yake na yeye aingie,ukiona makada wa chama chochote cha siasa wana kimbilia ikulu ujue wamechoka kazi wanatafuta kupumzika bila gharama, pia ni dalili za kuwa chama husika hakina mwenyewe tena watoto wazee vijana wote wana pigana vikumbo kugombea uongozi wa chama ujue nidhamu na maadili sio kigezo tena nawaombea mwisho mwema wote.

    mdau.

    Dodoma.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2015

    Anony acha zako bana, polisi kwa tz ni rafiki tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2015

    Wacha wagombee kama wanaona wanaweza wameona kizungu wanakijua, kuongiza wananchi na kuongea na mataifa mengine wanaweza kwa nini wasijitoe wacha waombe kazi. Sijui kama Kamati kuu ina kompyuta ya kutema wale wasiokuwa na vigezo vinavyotakiwa, kabla haijaingia kwenye usaili.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2015

    Hawa ndio viongozi tunataka kumrithi JK hakuna longolongo kazi tu. Hongera waziri chikawe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...