Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angellah Kairuki akisisitiza namna
mabaraza ya ardhi yanavyopaswa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria,
kanuni na taratibu zilizowekwa, wakati wa mkutano wa Waziri wa wizara hiyo na wananchi wa kata ya Makongo leo jijini Dar
es salaam. Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William
Lukuvi na wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kata ya Makongo Deusdedith Mtiro.
Meya wa Manispaa ya
Kinondoni Yusuph Mwenda akimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi William Lukuvi na ujumbe wake kwa kuahidi na kusisitiza kuwa kufanikiwa
kwa mradi wa Makongo kutahamasisha mpango wa ushirikishwaji wa wananchi katika
kuendeleza ardhi na kuwa na makazi bora ambapo kufanikiwa kwake kutahamasisha
mpango huo kutekelezwa maeneo mengine ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na akiongea na wananchi wa Kata ya
Makongo Manispaa ya Kinondoni (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya
Mpango Shirikishi wa kuendeleza ardhi na makazi ya wananchi kwa kushirikiana na
Serikali.
Mkazi wa Makongo juu Bi
Ritha Mbotto akimuuliza swali Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
William Lukuvi (hayupo pichani) wakati mkutano na wanchi wa kata ya Makongo
Manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwandishi wa habari
wa TBC Edward Kondela.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...