UN 12
Baadhi ya watu wenye ulemavu wakipita na mabango yenye ujumbe katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa maandamano kwenye maadhimisho ya Siku yao ambayo inalenga kutoa elimu ya kupinga matendo maovu wanayofanyiwa na watu wenye nia mbaya.(Picha na modewjiblog)

Na Mwandishi wetu, Arusha

MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodgriguez amepongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kushawishi dunia siku ya kukumbuka watu wenye ulemavu wa ngozi duniani.

Alisema dhana ya Juni 13 ilianzia Tanzania kwa mshikamano kati ya serikali ya Tanzania na mashirika yasiyo ya kiserikali kama Shirika la Under the same sun (TAS).

Alisema kutokana na bidii walizoonesha Novemba 18,2014, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha siku hiyo kuadhimishwa duniani kote kila ifikapo Juni 13
Akihutubia kabla ya rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi kuzungumza, Rodgriguez alisema dunia inapaswa kuangalia kwa makini maisha ya walemavu wa ngozi na kuzuia ukatili dhidi yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...