Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akionyesha kabrasha lenye
Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM mara baada ya kukabidhiwa
na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM wa Idara ya
Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu mkoani Dodoma leo.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu kabla ya kuchukua
fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Dodoma.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya
Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu kushoto akimkabidhi
fomu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma moja ya fomu
aliyokabidhiwa leo.
Hongera sana Dr. John Magufuri, MUNGU akubariki sana, yakupasa ufunge na kuomba ili BWANA YESU akupe kibali cha kuteuliwa. CCM wakitaka wapate urais kilaini zidi ya UKAWA wanatakiwa wamteue Dr. John Magufuri au Prof. Mark Mwandosya. Si yule kampeni meneja, "chama kwanza urafiki baadae".
ReplyDeleteHapa ...hata mie ninaewachukia sanaaaa naweza geuka nyuma na kuangalia vizuri......
ReplyDeleteCOUNT ON MY VOTE!!!!!
ReplyDeleteMnaoomba kazi ya kuongoza nchi hii kimya kimya na wale wanaotumia mbwembwe mnakaribishwa kuomba kwa unyenyekevu. Tutachunguza mambi yenu na nia zenu tuchague mwisho wa siku tutachagua mmoja wenu, na kuwashukuru wote waliotangaza nia na kugombea kwa njia mbalimbali. Tunawashukuru kwa kuthubutu, atakayechaguliwa OKtoba tunamatarajio makubwa ya kupiga hatua za maendeleo.
ReplyDeleteEh Mungu tunaomba uchaguzi wa amani usiokuwa na rabsha. Mungu mwenye enzi yote tunaomba pia utupatie kiongozi makini mwenye kuitakia nchi hii mema na maendeleo ya watanzania wote.
Huyu mchapa kazi anaonekana akipewa anaweza kuhamasisha watanzania kuleta maendeleo makubwa.
ReplyDeleteTunataka watu kama hawa
ReplyDeleteSafi sana mzeee
ReplyDelete