MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari ameungana na mamia ya wananchi katika kijijicha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo kufanya shughuli za awali za ujenzi wa chanzo kipya cha Maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Zoezi hilo lilo anza majira ya saa 3 asubuhi na kumalizika majira ya saa 12 jioni ilishuhudiwa Mbunge Nassar akishiriki kazi za mikono ikiwemo kubeba mawe na kuayapanga katika eneo la mto kwa ajili ya ujenzi wa chanzo hicho.
Akizungumza katika eneo hilo Mhe. Nassari alisema lengo la ujenzi wa chanzo hicho kipya ni harakati za kuokoa mazao kwa baadhi ya mashjamba ambayo yameanza kukauka kutokana na kukosekana kwa maji ya kutoshja.
“Nilijitolea kulipia malori matatu kwa siku nzima kufanya kazi hii na ununuzi wa nyaya maalum (chain link) kwa ajili ya kufungia/kujengea Mawe kwenye eneo ambalo chanzo cha maji haya kinaanzia lakini pia kwa sababu ilikuwa ni kazi ya kutwa nzima tulihakikisha hakuna anayeondoka katika eneo hili hivyo tuliamua kuchinja mbuzi ,tukapika ugali  na kazi ikaendelea”alisema Mhe.Nassari.
Mhe. Nassari aliwashukuru vijana zaidi ya 300 pamoja na kina mama waliofika katika zoezi hilo kwa lengo la kuendelea kumtia moyo.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki  Mhe. Joshua Nassari akiwa amepanda kwenye Lori lililokuwa likibeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji kwa ajili ya kumwagilia katika kijiji cha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Mhe Joshua Nassari akishirikiana na wananchi katika kijiji cha Karangai kuweka mawe katika chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Mbunge Nassari akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo hilo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2015

    Dah Dogo anajitahidi sana kushiriki shughuli za kijamii... Hongera Mh...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2015

    Jamani, Mbunge kudandia Lori tena ina husu? let us be realistic and not pretending, kwanza anahatarisha maisha yake, likifeli break itakuwaje hapo. I am just thinking aloud!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2015

    Huyu ni mbunge asiejielewa na vilevile kupotosha jamii kuhusu usalama. Hebu fikirieni mbunge kadandia lori je,mtu ambaye hana elimu kabisa ya usalama si atadandia kwenye tairi.wewe nasari ni mfano mbaya sana kwa jamii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...