Na Issa Sabuni, WKCU 
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira amepongeza hatua iliyofikiwa katika ya Serikali ya Tanzania chini ya Shirika la Uchumi na Maendeleo la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) na Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka nchini Poland akisifu kuwa hatua hiyo ni ya muhimu katika kuhakikisha Tanzania inaongeza tija na uzalishaji katika kilimo lakini pia inapunguza matumizi ya jembe la mkono. 
Waziri Wasira alipongeza hatua hiyo, mara baada ya kukutana na Bwana Karol Zarajczyk, ambaye ni Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka nchini Poland. 
Waziri Wasira alisema hii ni hatua njema kwani, mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea Kampuni ya Ursus mapema mwaka huu, wawekezaji hao walikubali wazo la kushirikiana Kampuni ya SUMA JKT kwa ajili ya kuunganisha matrekta hapa nchi badala ya kuyaleta yakiwa yameshaunganishwa ambapo gharama yake ni kubwa zaidi, ambapo wakulima wengi watashindwa kumudu gharama ya kuyanunua. 
 “Hatua ya Kampuni ya Ursus kukubali kuja Tanzania na kuwekeza kwa ushirikiano na SUMA JKT ni ya kupongezwa na kuungwa mkono, kwani itaiwawezesha wakulima wa Tanzania na wa Ukanda wa Afrika Masharikai kupata matrekta bora lakini pia, Kampuni hii ina uzoefu katika utengenezaji wa matrekta ya aina mbalimbali” Alisema Waziri Wasira. 
“Kufunga matrekta hapa nchini ni nafuu kuliko kuagiza matrekta yaliyokwisha fungwa, nawaomba tu mara baada ya Mkataba kusainiwa kati ya pande hizi mbili basi utekelezaji uanze mara moja na mimi kama Waziri wa Kilimo nitahakikisha, mnaazna kabla ya mwaka 2015 kuisha” Alikaririwa Waziri Wasira. 
Waziri Wasira alimueleza mgeni wake kuwa, maendeleo katika Sekta ya kilimo hayawezi kupatikana kama nchi na wakulima wadogo wataendelea na matumizi ya jembe la mkono na alimuhakikishia Mtendaji huyo Mkuu wa Kampuni ya Ursus ambaye yupo nchi pamoja na ujumbe wake ili kutiliana sahini ya utekelezaji huo katika ya Kampuni yake na SUMA JKT kwa ajili ya kuanza kufunga matreka madogo, ya kati na makubwa kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kibiashara na kuhakikisha matrekta, yanapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu. 
Aidha utekelezaji wake utawahakikishia, wakulima wadogo, wa kati na wakubwa ambao watanunua matrekata hayo kuwa na uhakika wa kupata huduma ya matengenezo na upatikanaji wa vipuri. 
Waziri Wasira aliongeza kuwa mara baada ya mkataba kusainiwa kati ya SUMA JKT na Kampuni ya Ursus, hatua inayofuata ni utekelezaji wake kuanza mara moja, Waziri aliongeza kuwa sehemu, itakayotumika kama karakana ya ufungaji wa matrekta hayo, ilipo karakana ya kilichokuwa, kiwanda cha kufunga magari aina ya Scania, TAMCO, Kibaha katika Mkoa wa Pwani.

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira akiwa na mgeni wake, Bwana Karol Zarajczyk, Mtendaji Mkuu na Rais wa Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus ya nchini Poland, wakati wa mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa Waziri, leo alasiri, Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...