Sehemu ya Umati wa wakazi wa wilaya ya Kwimba na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara,Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu,Ndugu Kinana alikemea tabia ya
wapinzania kuwahadaa vijana nchini kuwa wakiingia madarakani wataweza
kuwatekelezea kila kitu,aidha aliwataka vijana wa kitanzania kuacha
kabisa kuhadaika na baadhi ya Wanasiasa ambao wamekuwa wakiwapotosha na
kuamini kila kitu kitapatikana bila kufanya kazi na kujituma.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa
hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani Kwimba, ambapo
aliitaka jamii wakiwemo mabalozi wa mashina kuimarisha ulinzi kwa watu
wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO), ili kuepusha mauaji dhidi yao.
Wananchi
wilaya ya Kwimba wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara kwenye
Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa
yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa
akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo.
Mbunge wa Jimbo la Kwimba,Mh., Shanif Mansoor akiwahutubia Wananchi katika
mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo,
wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la
Kwimba jioni ya leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA katika Kijiji cha Ilula kata ya Ilula wilayani Kwimba,ndugu AmaraMateremki akizungumza baada ya kuamua kukihama chama hicho na kuijunga na CCM wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akionesha baadhi ya kadi za wafuasi wa chama cha CHADEMA kuhamia CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akikabidhi msaada wa baiskeli kwa watu wenye ulemavu Mjini Ngudu. Msaada huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor pichani shoto.
Mmoja wa viongozi kutoka kikundi cha akina mama kiitwacha UAMSHO akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana mara baada ya kukabidhiwa vyerehani vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...