Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za Chadema kutoka kwa vijana 20 waliojiunga na CCM na wanachama wapya zaidi ya 1520 walipewa kadi zao za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Sumve. Katika ziara yake kwenye jimbo la Sumve Katibu Mkuu wa CCM amepokea kadi 48 kutoka Chadema ikiwa 28 zilizorudishwa katika kijiji cha Goloma kata ya Mwadu.
kadi za Chadema kutoka kwa vijana 20 waliojiunga na CCM na wanachama wapya zaidi ya 1520 walipewa kadi zao za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Sumve.
Wananchi wa Kata ya malya wakionyesha Bango kubwa lenye ujumbe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana lenye madai ya kudhulumiwa viwanja ambavyo tangia walipie miaka mitatu sasa hawajapata viwanja,Katibu Mkuu wa CCM alikuwa njiani kuelekea Nyambiti ndipo wananchi hao walimsimamisha barabarani na kutoa kero zao.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungunza na wakazi wa kata ya Malya ambao wanadai viwanja vyao walivyovilipia miaka mitatu iliyopita,lakini mpaka sasa wananchi hao hajakabidhiwa,Ndugu Kinana ameipa muda wa miezi miwili na ushehe kuwa ifikapo septemba 1,2015 ,Halmashauri ya wilaya ya Sumve ihakikishe imelitatua tatizo hilo na wananchi kupewa viwanja vyao. Katibu Mkuu wa CCM alikuwa njiani kuelekea Nyambiti ndipo wananchi hao walimsimamisha barabarani na kutoa kero zao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Sumve,Mh Richard Ndassa,mara baada ya kuzindua huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji cha Mwabilanda wilayani Kwimba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia sehemu ya kunyweshea maji mifugo katika kijiji cha Kishilili, ambapo Ng'ombe zaidi ya 800 hupata huduma ya maji safi na salama katika mradi ambao pia husaidia kaya 102 kupata maji safi na salama katika kisima kinachotumia mfumo wa jua (solar power).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...