Na Bashir Yakub.
Suala la mirathi popote linapotokea hutokea iwapo kuna mtu amekufa na ameacha mali . Mtu akishakufa akaacha mali hata kama hakuna ndugu wa kurithi suala la mirathi lazima liibuke. Huibuka kwakuwa lazima zile mali ziende pahali iwe kwa mtu au kwa mamlaka. Hata hivyo suala la mirathi huibua hisia zaidi hasa panapokwa hamna wosia. Marehemu asipoacha wosia lakini akaacha mali mambo huwa sio mepesi sana labda iwe vinginevyo.
Ifahamike kuwa mirathi huhusisha mambo mengi. Lakini pia huhusisha sheria nyingi. Sheria za kiislam huhusika, sheria za kimila huhusika na pia sheria za nchi ambayo ni sura ya 352.
1.USIMAMIZI WA MIRATHI KAMA KUNA WOSIA.
Kama marehemu ameacha wosia basi ni vema kuangalia wosia huo umemtaja nani awe msimazi wa mirathi. Hili ni muhimu watu walijue hata wale walioandika wosia tayari au wanaotarajia kuandika wosia. Wengi wamekuwa wakiandika wosia na kugawa mali lakini wakisahau kuteua na kumtaja msimamizi wa mirathi wakiamini kuwa kila mtu atakapochukua chake mambo yataishia hapo.
Laa hasha mambo si mepesi kiasi hicho. Kwa hiyo yafaa kuangalia nani ametajwa kama msimamizi wa mirathi katika wosia na huyu ndiye atakuwa msimamizi wa mirathi. Ikiwa wosia upo lakini haukumtaja msimamizi wa mirathi basi taratibu za kimahakama nitakazoeleza hapa chini zitafuata.
2. KUMTHIBITISHA MSIMAMIZI WA MIRATHI MAHAKAMANI.
Ikiwa wosia umemtaja msimamizi wa mirathi basi hilo tu halitoshi. Sheria inataka msimamizi wa mirathi athibitishwe pia na mahakama. Hii ni kwasababu mahakama hutoa hati maalum kwa aliyethibitishwa kuwa msimamizi wa mirathi ambayo hutum ika sehemu zote za kisheria kwa mfano kuchukua hela za marehemu benki, kuchukua hisa za marehemu, kuuza na kununua mali za marehemu,kubadilisha vitu kama hati na kila kitu ambacho huhusisha taratibu maalum za kisheria. Kwakweli isingewezekana kutumia wosia kwa kuuonesha kila ofisi unayoingia katika kufanya michakato hii yote. Na hapa ndio mahitaji ya kuthibitishwa na mahakama na kupata hati maalum ambayo ni kama utambulisho yalipotokea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...