Mwenyekiti wa Afya Sacos Othman Mussa Juma akitoa hutuba ya ufunguzi wa
Mkutano Mkuu wa Ushirika huo uliofanyika Ukumbi wa Ecrotanal Mjini Zanzibar. Wajumbe
wa Mkutano huo walizimia kuongeza Akiba ya shilingi elfu 30 kutoka elfu 10 kwa
mwezi ili kuzidi kujikwamua na Umaskini.
Mgeni Rasmi wa Mkutano huo ambaye ni Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Madawa
Zanzibar Zahran Ali Hamad akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Ushirika wa Afya
Sacos. Katika Mkutano huo aliwaomba kuzidisha mashirikiano miongoni mwao.
Baadhi ya Wanachama wa Ushirika wa Afya Sacos wakisikiliza hutuba ya
ufunguzi ya mgeni rasmi(hayupo pichani) katika Mkutano wa mwaka wa Ushirika
huo.
Katibu Mkuu wa Ushirika wa Afya Sacos Kassim Issa Kirobo akitoa nasaha
zake katika Mkutano huo ambapo aliwaahidi kusimamia vyema Ushirika huo ili
utimize lengo la kujikwamua na Umaskini.
Mmoja wa wanachama wa AFYA SACOS Makame Mussa akichangia katika mkutano
huo ambapo aliwasihi Viongozi wake kuwa waadilifu ili Ushirika wao uweze
kuwaletea maendeleo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...