Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel leo imezindua mnara wa mawasiliano katika wilaya ya
Ikungi mkoani Singida ambao utasaidia upatikanaji wa mawasiliano na
pia kuboresha ubora wa mtandao kwa wakazi wa wilayani hapo na maeneo
ya jirani.
Meneja wa kanda ya kati wa Airtel, Bwana Stephen Akyoo, alisema Mnara
huo mpya wa mawasilino ni moja kati ya mikakati ya kampuni yake
kujitanua zaidi na kuboresha mtandao wa mawasiliano, huku wakiendelea
kuangalia namna ya kuendelea kufanya huduma zao kuwa za gharama nafuu
na kupatikana kwa wakazi wote nchini. Mnara huo mpya wa mawasiliano
utawafaidisha wakazi zaidi ya 15,700 ambao ni wakazi wa wilaya ya
ikunga pamoja na vijiji vitano vya jirani vya Mpugizi, Mlandala,
Kaugeri, Mduguyu na Kimpuma.
“Tunaamini moja kati ya vikwazo vikubwa vya mawasiliano bora Tanzania
ni upatikanaji wa huduma za mawasiliano na ndio dhamira yetu kubwa ya
kuhakikisha tunapanua wigo wetu kwa kuzindua minara ya mawasiliano na
kuwezesha maeneo yaliyo pembezoni mwa nchi kufikiwa na kupata
mawasiliano bora.
Tumekuwa tukitoa kipaombele katika kuboresha
upatikanaji wa huduma za mawasiiano katika maeneo ya vijijini
tukiamini kwa njia hii tutaweza kuboresha shughuli za kilimo, uvuvi,
madini pamoja na shughuli nyingine za kibiashara ambazo ndizo nguzo
ya kukua kwa uchumi wan chi yetu. Leo wakazi wa kata ya Mwaru
wataweza kunganishwa na mtandao wa kisasa, huduma za kupiga simu
pamoja na huduma za Internet nakufurahi huduma zetu nyingi za kibunifu
ikiwemo huduma ya Airtel Money.”
Aliongeza kwa kusema ikiwa ni njia ya kuwahudumia wateja wa maeneo
haya vyema, Airtel imesajili mawakala zaidi ya watano wa huduma ya
Airtel Money katika kijiji cha Mwaru watakaoungana na mawakala wetu
zaidi ya 45,000 nchini katika kuhakikisha huduma ya pesa kupitia simu
za mkononi inapatikana wakati wote.
Akiongea wakati wa uzinduzi, Diwani wa kata ya Mwaru, Bwana Omary
Hassan Mgisa, akimwakilisha Mkuu wa wilaya, aliwapongeza Airtel kwa
kuwafikishia mawasiiano kwani hapo awali watu wengi walikuwa na
matatizo makubwa ya mawasiliano na kukwamisha shughuli zao kwa kiasi
kikubwa. Tunafurahi kwa Airtel kuleta mawasilino haya karibu na watu
kwani huduma za mawasiliano ni chachu kubwa katika kukuwa kwa uchumi.”
Napenda kuwashauri wakazi wa hapa kujisajili katika mtandoa wa Airtel
nakutumia huduma zao kama vile Airtel Money kufanya miamala ya kifedha
kwaajili ya familia zao na biashara zao kwa haraka na usalama zaidi.
“nikiwa kama kiongozi wa eneo hili nahaidi kushirikiana kwa dhati na
kuhakikisha makampuni kama Airtel yanayojali wateja wake, wanapata
mazingira mazuri ya kuwekeza ili kuendelea kutoa huduma bora na nyingi
zaidi kwa jamii” aliongeza Mgisa
Meneja wa kampuni ya Airtell kanda kati bwana Martin
Kilasara, akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Omary Hassan Mgisa Diwani wa kata
ya Mwaru tarafa ya sepuka Wilayani Ikungi Singida Wakati wa Uzinduzi wa
Mnara wa Airtel katika kijiji cha mwaru.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa
mnara wa airtelOmar Hassan Mgisa Diwani wa kata ya Mwaru akikata utepe
wakati wa uzinduzi wamnara wa airtel katika kijiji cha mwaru wilayani
ikungi mkoani Singida jana wakati wa uzinduzi wa mnara huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...