Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula leo jioni siku ya Jumapili July 12, 2014 alijumuika na wanajumuiya ya Kiislam ya DMV (TAMCO) katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na jumuiya hiyo na kutumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.

Katika hotuba yake. Mhe. Liberata Mulamula  aliwakuwakumbusha alipokuja kwa mara ya kwanza kulitumikia Taifa kama Balozi wa Tanzania nchini Marekani , Jumuiya hiyo ndio iliyomkaribisha kwa mara ya kwanza hapa DMV na leo nimerudi tena kuagana nanyi rasmi. Mhe. Liberata Mulamula aliwashukuru TAMCO kwa ushirikiano na mshikamano wao na kuzitaka Jumuiya zingine za Watanzania ziige mfano wao kwani TAMCO ni jumiya ya Kiislam iliyoimara, isiyotetereka na yenye uongozi makini. Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliushukuru uongozi wa TAMCO kwa kumkaribisha aje azungumze na Watanzania wanajumuiya ya TAMCO na kutumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.

Uongozi wa TAMCO ulimuzawadia Mhe. Balozi Liberata Mulamula zawadi na yeye kutoa mchango wake wa mwaka kwa jumuiya hiyo inayo wakubali Watanzania wote bila kubagua rangi, kabila wala dini.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Watanzania DMV (TAMCO)Ustadh Ally Mohamed akimlaki Mhe. Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulaula mara tu alipowasili kwenye ukumbi wa park iliyopo Silver Spring, Maryland nchini Marekani alipokuja yeye Mhe. Balozi akiambatana na mumewe Eng. George Mulamula (hayupo pichani) na mwanae Alvin Mulamula (kulia) kujumuika na wanajumuiya hao katika futari ya pamoja na kutumia futari hiyo kuwaaga rasmi. Picha zote na Kwanza Production na Vijimambo Blog.
 Mtunza fedha msaidizi wa TAMCO. Bi. Asha Hariz(kushotao) akiongozana na Mhe. Liberata Mulamula kuelekea ukumbini siku ya Jumapili July 12, 2015 siku Mhe. Balozi alipopata mwaliko wa Jumuiya hiyo wa kufuturu pamoja na kuwaaga rasmi.
Mwenyekiti wa TAMCO ustadh Ally Mohamed akiongea machache na baadae kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuongea na wanajumuiya.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...