Askari Polisi kadhaa, mgambo na raia wameuwawa kikatili na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Sitakishari, Ukonga, jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo. Silaha kadhaa pia inasemekana zimeporwa na majambazi hayo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu yupo eneo la tukio muda huu na ametangaza msako wa nguvu kuwasaka waliohusika na tukio hilo na kukomboa silaha zilizoporwa.
Kikosi kazi cha Globu ya Jamii kipo eneo la tukio kukusanya taarifa sahihi na rasmi kwa picha na video ambazo mtazipata baada ya muda si mrefu ujao.
Kikosi kazi cha Globu ya Jamii kipo eneo la tukio kukusanya taarifa sahihi na rasmi kwa picha na video ambazo mtazipata baada ya muda si mrefu ujao.
Mambo gani haya?
ReplyDeleteSio majambazi hawa watakua nu wale magaidi wanaovamia vituo vya polis
ReplyDeleteJAMANI UZEMBE MWINGI NDANI YA JESHI LA POLISI, INTELIGENSIA YA WAZI (OPEN INTELLIGENCE) INAONYESHA WAZI KUWA VITUO VIDOGO VYA POLISI HASWA MAENEO YA MBALI NA MJI NA VYENYE ASKARI WACHACHE VIKO KATIKA HATARI/RISK YA KUVAMIWA HASWA USIKU. PIA ASKARI HAO HUWA WANALALA KAZINI NA HAWAKO MAKINI/ALERT KWAMBA LOLOTE LINAWEZA TOKEA SAA YEYOTE. POLISI KUWENI MAKINI NA WAELEVU MBELE YA UELEVU/AHEAD-OFF WA MAJAMBAZI. MAMBO YAMESHAHARIBIKA NCHINI - JOE BURA, DAR
ReplyDeleteHii inatisha na kusikitisha, ikiwa Polisi ndo tunaona sehemu salama Leo vituo vinavamiwa siye raia tutapona kweli?
ReplyDeleteNi kweli polisi waongeze umakini zaidi
ReplyDeleteukiona vituo vya polisi vinavamiwa na silaha kuibiwa basi jua kuna siku vita itatokea tz.. watu wanaiba na kujilinbikizia silaha tayari kwa vita..za kuambiwa changanya na za kwako-JMK
ReplyDeleteRaia tuwe na ushilikiano na vyombo vya ulinzi ilikutoa taarifa za watu wasio fahamika mapema
ReplyDelete