Posted: 08 Jul 2015 11:54 AM PDT
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Alli Hassan Mwinyi, akikagua maonyesho ya kazi zinazofanywa na manispaa ya Kinondoni.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni , Yusuph Mwenda akimkabidhi jezi ya timu ya soka ya Kinondoni Municipal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi kama ishara ya kuwa mlezi wa timu hiyo
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Alli Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti na na nishani ya utumishi uliotukuka Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda wakati wa sherehe zabkufunga baraza la manispaa hiyo
Rais Mstaafu wa awamu ya pili , Alhaji Ally Hassan Mwinyi, akimkabidhi cheti cha utumishi uliotukuka katika baraza la madiwani Mkurugunezi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, wakati wa hafla ya kuvunja baraza la madiwani la Manispaa ya Kinondoni

Na Mwandishi wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeliahirisha rasmi Baraza la Madiwani ambapo mgeni rasmi katika kuahirisha Baraza hilo alikuwa mheshimiwa Rais mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.
Shughuli hizo zilianza kwa kikao cha baraza cha kawaida cha kupokea taarifa ya utekelezaji ambapo baada ya hapo aliwasili mgeni rasmi Mheshimiwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kufuatiwa na tukio la kupita katika mabanda maalum yaliyoandaliwa yakionyesha shughuli za kila idara na kupata maelezo ya shughuli zinazofanywa na idara hizo pasitisha moja na mafanikio mbalimbali katika idara hizo.Baada ya mgeni rasmi kupita katika mabanda hayo na kupata maelezo ndi[po kilianza kikao rasmi cha baraza cha kusitisha rasmi baraza hilo ambapo lilianza kwa ufunguzi wa sala na kisha utambulisho uliofanywa na Mstahiki Meya Yusuphu Mwenda kabla ya wawakilishi mbalimbali wa vyama vya siasa kutoa neno.

Akiongea mkurugenzi wa jiji alilipongeza baraza la Madiwani na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondonikwa kazi nzito waliyoifanya ambayo Tanzania nzima wanaikubali ikiwepo ukusanyaji mzuri wa mapato na kumalizia kuwa Manispaa hii ni mfano mzuri wa kuigwa na Mstahiki Meya ni Meya wamfano kwa Tanzania nzima.Akiongea katika kikao hicho mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni alilishukuru Baraza la madiwani kwa ushirikiano wao katika kutekeleza shughuli za maendeleo kwa Manispaa hii ambapo ni mengi sana yaliyotekelezwa na mengine kutokana na muda bado hayakuweza kutekelezeka,lakini ameahidi kuyatimiza yale ambayo wameyabariki yafanyike likiwepo la kujengwa kwa mtambo wa kuchakata taka huko mabwepande ambapo tayari na mkataba umeshasainiwa wa kuanza kujengwa kwa mtambo huo kwa msaada wa Humburg city.
Mgeni rasmi alitoa medani na vyeti kwa madiwani na kwa baadhi ya watendaji akiwepo Mkurugenzi.Katika kuitambulisha timu ya KMC-FC ambayo ni timu ya Manispaa ya Kinondoni mgeni rasmi alikabidhiwa jezi ya timu hiyo yenye jina lake Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ,hali kadhalika madiwani pia walipewa jezi hizo kila mmoja zenye majina ya kila mmoja na mkurugenzi aliwaomba kuitangaza timu hiyo na kuisaidia kwa hali na mali .
Akiongea katika hafla hiyo Mstahiki Meya aliwashukuru wakazi wa kinondoni kwa ushirikano.kuhusiana na suala la maendeleo Meya alisema kumekuwa na ushiriki mpana wa wananchi katika maendeleo na pia uboreshwaji wa fedha za matumizi ya umma kwa kujenga mashule,barabara,mahospitali ambapo aliiongelea pia hospitali ya Mabwepande ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi,akiongelea upande wa mapato alisema pato limeongezeka sana kutoka bil.11 kutoka kipindi cha nyuma hadi kufikia bil.35 hivi sasa.Akiongelea suala la vibali vya ujenzi kwa sasa vimekuwa vikitolewa na kupunguza msongamano na nia ni kuhakikisha vibali vya ujenzi vinapatikana ndani ya wiki moja,kuhusu usafi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2015

    Mwandishi nafikiri ulikuwa unamaanisha "kuvunjwa na si kuhairishwa" kuna tofauti kubwa sana kati ya kuhairishwa naa kuvunjwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...