Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa nchini linawakumbusha wasanii wote nchini kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo wanapokwenda nje ya nchi kufanya maonesho au kushiriki shughuli yoyote ya Sanaa ili kuepuka matatizo na mikanganyiko mbalimbali inayoweza kujitokeza.

Kwa mujibu wa taratibu zilizopo, msanii yeyote anapokwenda nje ya nchi anapaswa kujaza fomu maalumu inayotolewa na BASATA na baadaye kupewa kibali bure (bila gharama yoyote) ambacho mbali na kueleza wapi msanii anaelekea kinaeleza kwa kina tarehe ya kuondoka kwa msanii na ile ya kurudi nchini.

Kutokana na kukua kwa sekta ya Sanaa nchini hususan muziki na filamu wasanii wengi wamekuwa wakipata fursa ya kwenda nje ya nchi kufanya maonesho na shughuli zingine za Sanaa hivyo suala la kufuata sheria, kanuni na taratizu za kupata vibali vya kwenda nje ya nchi ni muhimu sana ili kuhakikisha kwanza; safari zao zinakuwa na baraka ya moja kwa moja kutoka Serikalini, pili kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi za wasaniii wanaokwenda nje ya nchi, tatu usalama wa wasanii wetu na mwisho, kuwakabidhi bendera ya taifa kama ishara ya uwakilishi na ubalozi wa nchi yetu katika mataifa wanayoyatembelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2015

    Basata mkajipange upya, sababu zenu bado zina utata mkubwa tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2015

    SIASA ZA BASATA..NASEEB ABDUL KAWAUMBUA SANA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2015

    Kama msanii anaenda huko nje kwa gharama zake kwa nini apitie kwenu?
    Acheni sanaa iwe soko huria mambo ya ukiritimba "msanii apate Baraka toka Basata" yamepitwa na wakati.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...