Benki M, inayojulikana kimataifa na ambayo ipo katika benki 10 kubwa hapa nchini, imepata faida ya zaidi ya asilimia 25 katika faida kabla ya kodi kwenye nusu ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. 

Benki hiyo ambayo hivi karibuni ilijipatia tuzo ya Benki bora ya biashara Tanzania kwa mwaka 2015 iliyotolewa na International Banker nchini Uingereza, imepata faida kufikia Tshs. 11.51Billioni kabla ya kodi katika miezi sita ya mwanzo wa mwaka ikilinganishwa na Tshs. 9.18Billioni mwaka jana.
Akiongea kwenye wa mkutano na waandishi wa habari wakati wakitoa hesabu zao za robo ya pili ya mwaka, Naibu Mkurugenzi mkuu wa Benki M Bi. Jacqueline Woiso alisema kuwa benki M inaamini katika kutoa mahesabu yenye mchanganuo wa kina na pia kutoa mahesabu hayo mapema zaidi. “Katika robo zote 32 tokea kuanzishwa kwetu tumeweza kutoa hesabu zetu za fedha ndani ya siku saba za mwanzo wa mwezi unaofuata. 

Na pia hesabu hizo huwa na uwazi kabisa katika kuelezea kila kipengele, hilo hutufanya tuwe wa kipekee kabisa ukilinganisha na benki nyingine hapa nchini”. Alisema faida itokanayo na shughuli nyingine za kibenki (ukiondoa mikopo) imeongezeka kufikia Tshs 11.9Billioni hadi juni 2015, kutoka Tshs 8.841Billioni mwezi Juni mwaka 2014.

Katika kutafuta namna ya kuongeza wigo wa huduma, Benki hiyo inatarajia kuongeza mtaji kwa takribani Tshs 20Billioni kutoka kwa wanahisa wa Benki na kiasi cha Tshs 10Billioni kupitia katika soko la hisa kwa kushirikisha wawekezaji watakaopenda kuwekeza katika taasisi yetu. Haya yote kwa pamoja yatakamilika katika nusu ya pili ya mwaka huu.

“Kupitia hizi hisa stahili mtaji wetu halisi utaongezeka maradufu kwa zaidi ya kiwango cha asilimia 15” Bi. Woiso alisema. Sehemu kubwa ya mikopo inayotolewa na Benki M inalenga katika sekta ya viwanda na uzalishaji, Utalii,Ujenzi na makazi, mawasiliano pamoja na kilimo.

Benki M, ipo katika nafasi ya nane katika benki kubwa kwa upande wa mizania na pia ni ya sita katika benki zinazotengeneza faida, ilianzishwa mwaka 2007 kwa lengo la kutoa huduma yenye kiwango cha hali ya juu Africa na hilo limewezekana. Mwezi huu Benki M itafikisha miaka 8 toka kuanzishwa kwake. “Ni kiwango kizuri kwa benki inayokua kwa haraka kama hii yetu, ni kwa sababu ya jitihada zetu katika kutoa huduma iliyo bora zaidi ambayo imekua ikiwaridhisha wateja wetu” aliongeza Bi Woiso.

Mbali na kupata tuzo ya benki bora ya biashara kwa mwaka 2015, Benki M imejizolea tuzo nyinginezo pia za kimataifa hivi karibuni ikiwemo tuzo ya Benki bora katika sekta ya biashara za makampuni Afrika Mashariki na Benki bora inayoshiriki katika maendeleo ya jamii Afrika Mashariki zilitolewa na Banker Africa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...