Na Sultani Kipingo
Bingwa wa dunia wa masumbi
Floyd Mayweather (kushoto) amevuliwa mkanda wa WBO alioupata baada ya kumshinda Manny (kulia)
Pacquiao mwezi Mei Mwaka huu.
Uamuzi huo umekuja baada ya
bondia huyo mwenye umri wa miaka 38 kushindwa kuilipa shirikisho la ndondi la
WBO ada ya dola laki mbili kabla ya Julai 3, mwaka huu.
Hata hivyo Mayweather mwenyewe
alitegemewa kuutema mkanda huo, kufuatia ushindi wa pointi dhidi ya Pacquiao. Mmarekami
mwenzie Timothy Bradley ndiye ataepewa mkanda huo.
Baada ya kumshinda Pacquiao,
Mayweather alitangaza kwamba angeutema mkanda huo ili kuwapa fursa mabondia
wengine vijana kushinda mikanda.
“Kamati ya mashindano ya dunia
ya WBO hina jinsi ila kukoma kumtambua Bw. Floyd Mayweather Jr. kama bingwa wa
dunia wa uzito wa welterweight na tunamvua ubingwa huo”, taarifa imesema katika
mtandao wa wboboxing.com
Mayweather anategemea kuingia
ulingoni tena huko Las Vegas Septemba 12, mwaka huu ingawa bado hajataja
atapambana na nani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...