Mhe. Dkt. Titus Kamani (Mb) amefanya ziara katika Wilaya za Kiteto na Kilindi kukagua ujenzi wa malambo kwa ajili ya maji ya mifugo na binadamu. Malambo hayo yamegharamiwa na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika bajeti ya mwaka 2014/15. 
Lambo la Olpopong lililopo Wilaya ya Kiteto limegharimu Tshs.584 milioni. Aidha lambo la Kwamaliga lililopo Wilaya ya Kilindi litagharimu Tshs.1.25 bilioni. Mifugo zaidi ya 60,000 kutoka katika Vijiji vya Kimana, Ngabolona Ndaleta inatarajiwa kunufaika na lambo la Olpopong. 
Lambo la Kwamaliga litahudumia takribani mifugo 100,000 kutoka ndani na nje ya Wilaya ya Kilindi.
Mhe.Dkt. Titus Kamani (Mb) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi Bibi. Hadija Pori kuhusiana na kazi zilizofanyika na hatua iliyofikia katika ujenzi wa lambo la Olpopong.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Olpopong mara baada ya kukagua shughuli za ujenzi wa lambo.
Mhe. Dkt. Titus Kamani akiangalia lambo la Kwamaliga lilivyobomoka. 
 Mhe. Dkt. Titus Kamani akizingumza na wananchi wa Kijiji cha Kwamaliga baada ya kukagua eneo la ujenzi wa lambo. Picha na Elukaga Mwakipesile.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...