![]() |
Waziri wa zamani Daniel Yona akiituliza familia yake mara baada ya hukumu kutolewa leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam. |
![]() |
Waziri wa zamani Basi Mramba akiteta na mawakili wake baada ya kuhukumiwa leo mahakamani Kisutu. |
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Grey Mngonja (kushoto) ameachiwa huru bada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yake.
Pia Mahakama hiyo imewahukumu kulipa faini ya shilingi milioni 5 au kwenda jela miaka 2 zaidi baada ya kukutwa na hatia ya kuisababishia serikali hasara ya shilini bilioni 11.7.
Washitakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni iliyopata zabuni ya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini.
Hukumu hiyo imetolewa chini ya jopo la mahakimu watatu ambao ni Hakimu Saul Kinemela, Jaji Sam Rumanyika na Jaji John Utamwa aliyekuwa mwenyekiti wa jopo hilo baada ya kupitia ushahidi pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa na pande zote mbili katika kesi hiyo.
Kwa mara ya kwanza washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo mwaka 2008 wakikabiliwa na mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
kweli sharia ni msumeno, ila hilo la kuachiwa Papaa Msofe linanitatiza akili
ReplyDeleteVipi kuhusu hukumu ya kuchapwa viboko pia
ReplyDeletehukumu ya mabilioni miaka mitatu tu na huko jela kutakuwa na upendelea wa kufa mtu.tanzania aliyeiloga alikufa
ReplyDeletembona hukumu ndogo sana kial Maranda na Farijala wamekula mitano mitano ,wwao walikula million 200 tu sasa hao wa mabilion miaka mtatu tu?
ReplyDeleteMimi sielewi
Yaani kesi yaendeshwa kwa miaka saba kisha mtu anafungwa miaka mitatu jela na faini ya milioni tatu tu!Walau kajala alilipa milioni 13 na kuepuka kifungo kirefu ambapo aliekua mumewe anatumikia zaidi ya miaka 10 jela kwa kesi ndoogo.
ReplyDeleteMungi ibariki nji yetu
ReplyDeleteMungu ibariki Tanzania
ReplyDeleteMimi nilitegemea miaka 30 jela, kurudisha hayo mabilioni na viboko juu. Hapo mnawaambia na wengine wenye mawazo kama hayo bongo hakuna matata
ReplyDeleteNikweli kifungu kidogo lkn tumepiga hatua kubwa .
ReplyDeleteKuweza kumfunga mtu alie kuwa waziri nijambo kubwa na lakupongezwa sasa wengine kabla ya kufanya makosa watajishauri marambilimbili.
Mini ninaona tuipongeze serikali na tuipongeze Mahakama yetu kwa hatua kubwa walio piga hii.
Inaonekana tunakokwenda ni kuzuri kumbe minyangumu pia inaweza kufungwa.
movie ndo kwanza imeanza sterling ni mranba.. za kuambiwa changanya na za kwako...JMK
ReplyDeleteMAHAKAMA IEPUKE DOUBLE STANDARD.KOSA DOGO LINAKUWA NA HUKUMU KUBWA,INAKUWAJE KOSA LA MABILIONI WATU WAHUKUMIWE MIAKA MITATU TU
ReplyDeleteMIE NAONA WANGEFILISIWA MALI ZAO KUFIDIA PESA WALIZOIBA ILI IWE FUNDISHO KWA VIGOGO WENGINE, AU NANI ATALIPA HIZO BILIONI 11
ReplyDelete