Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex
Msama
MUIMBAJI wa Muziki wa Injili
anayekuja kasi katika muziki huo, Danny Bulenge amesema anakidhi kuwa mmoja wa
watakaomsindikiza mwenzake Bonni Mwaitege uzinduzi unaotarajia kufanyika Agosti
2 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Bulenge anakidhi
kumsindikiza Mwaitege anayetarajia kuzindua albamu tatu ambazo ni moto wa
kuotea mbali katika muziki huo.
Bulenge alisema hivi sasa
anaendelea na mazoezi kwa lengo la kufikisha ujumbe wa neno la Mungu na kuahidi
kusindikiza vilivyo albamu hizo tatu kwa staili ya aina yake.
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex
Msama, Bulenge ni mmoja wa wataungana na Mwaitege katika uzinduzi huo.“Uzinduzi wa
albamu tatu za Bonny Mwaitege unatakiwa kufanyika kwa maandalizi ya hali
ya juu ambayo yanafanyika kwa mfumo wa
kisasa,” alisema Msama na kuongeza.
“Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa
ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa yamefanywa kwa ustadi
mkubwa hasa hatua za mwisho za rekodi ya
albamu hizo inayomaliziwa jijini Mwanza
na baadaye Nairobi,” alisema Msama.
Msama alisema sambamba na
muimbaji huyo, mikoa mbalimbali imeonesha nia ya kutaka uzinduzi wa albamu
hizo. Aidha Msama alitoa wito kwa
mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania kujiandaa kupata neno la Mungu kupitia
muimbaji huyo. Bonny Mwaitege anatamba
na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako
na njoo uombewe na Yesu yupo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...