Wananchi na Wafuasi wa chama cha Mapinduzi CCM wakiwapokea kwa shangwe Mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea mwenza Mh.Samia Suluhu Hassan mapema asubuhi hii mara baada ya kuwasili mjini Unguja -Zanzibar kujitambulisha kwa chama na Wananchi kwa ujumla.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la wazi pamoja na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye mitaa ya Michenzani Zanzibar.

Mhe. Magufuli aliwasili Zanzibar kwa lengo la kutambulishwa kwa wanachama wa CCM Zanzibar akiongozana na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan ambapo wote kwa pamoja walipata kuwasalimia wananchi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.


 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli nje ya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kwenye sherehe fupi ya kutambulishwa wagombea wa CCM kwa wanachama wa CCM.

 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John P.Magufuli pamoja na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiomba dua mbele ya kaburi la Hayati Abeid Aman Karume muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.

 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Magufuli akiwasalimu wananchi waliojitokeza kwenye sherehe fupi za kumtambulisha kwenye viwanja vya Afisi Kuu CCM Zanzibar.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...