MWIMBAJI wa Kimataifa anayeishi, Kenya Faustine Munishi
anatarajia kumsindikiza mwenzake Bonny Mwaitege anayetarajia kuzindua albamu
tatu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama
Promotions, Alex Msama, Munishi ataungana na Mwaitege, uzinduzi utakaofanyika
Agosti 2 mwaka huu.Msama alisema Munishi ni
mojawapo ya watakaomsindikiza mwimbaji
huyo kwa sababu hivi sasa sambamba na Kilahiro na Kwaya ya Wakorintho wapili.
“Uzinduzi wa
albamu tatu za Bonny Mwaitege unatakiwa kufanyika kwa maandalizi ya hali
ya juu ambayo yanafanyika kwa mfumo wa
kisasa,” alisema Msama na kuongeza.
“Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa
ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa yamefanywa kwa ustadi
mkubwa hasa hatua za mwisho za rekodi ya
albamu hizo inayomaliziwa jijini Mwanza
na baadaye Nairobi,” alisema Msama.
Msama alisema sambamba na
muimbaji huyo, mikoa mbalimbali imeonesha nia ya kutaka uzinduzi wa albamu
hizo.Aidha Msama alitoa wito kwa
mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania kujiandaa kupata neno la Mungu kupitia
muimbaji huyo. Bonny Mwaitege anatamba
na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako
na njoo uombewe na Yesu yupo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...