TIMU ya soka ya vijana chini ya miaka 11 ya FC Vito Kilwa ya Kilwa mkoani Lindi, imemaliza mechi za hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Helsinki Cup 2015 kwa kishindo, baada ya kushinda mechi nne na kutoka sare moja, hivyo kumaliza ikiwa kinara wa Kundi BJ/11 ikiwa na pointi 13.
Zaidi ya timu 1,200 zinashiriki michuano hiyo ya nne kwa ukubwa miongoni mwa michuano ya vijana barani Ulaya, inayoendelea kushika kasi jijini Helsinki nchini Finland, ambako Tanzania inawakilishwa na FC Vito Kilwa inayomilikiwa kwa ubia kati ya Sports Development Aid (SDA) ya Lindi na Liike Finland ya Finland.
FC Vito ilifungua michuano hiyo Jumapili kwa kuibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya FC Reipas, kabla ya Jumatatu asubuhi kuizabua Wilpas-FC Halikko kwa mabao 4-1. Katika mechi ya pili jioni ya Jumatatu, FC Vito iliichapa NJS Keltainen FC kwa mabao 5-0.
Moto wa FC Vito ya Kilwa mkoani Lindi katika michuano hiyo ulipunguzwa makali ya ‘kuwaunguza Wazungu’ mapema Jumanne asubuhi, wakati waliposhuka dimbani na kubanwa mbavu hivyo kuambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Euran Pallo.
Jioni ya Jumanne, FC Vito wakiwa chini ya kocha Mohamed Mtule walishuka dimbani kuumana na HJK Kannelmäki Sininen na kushinda kwa mabao 4-0, hivyo kutinga hatua ya mtoano, ambako leo Jumatano wanaumana na mshindi wa pili Kundi P/II ambayo ni NJS Sininen kwenye dimba la Käpylä 9B.
Zaidi ya timu 1200 zinashiriki michuano hiyo ya nne kwa ukubwa miongoni mwa michuano ya vijana barani Ulaya, ambako Tanzania inawakilishwa na FC Vito Kilwa, ya Kilwa mkoani Lindi.
FC Vito Kilwa wakiwa katika picha ya pamoja na FC Jazz baada ya mechi ya fainali ubingwa wa michuano midogo ya maandalizi kuelekea Kombe la Helsinki. FC Jazz ilishinda kwa mabao 3-0.
FC Vito Kilwa wakiwa nchini Finland.
FC Vito wakipozi kwa picha nchini Finland kabla ya moja ya mechi za maandalizi ya Helsinki Cup 2015.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania - TFF, Boniface Wambura katikati akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa FC Vito baada ya hafla ya kuwaaga ubalozi wa Finland Dar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...