Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea wakati wa ufunguzi wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars kwa viongozi wa mikoa iliyofanyika leo (Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi na Kushoto ni Mwenyekiti msaidizi soka la vijana wa TFF Khalid Abdallah.
Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Salim Madadi akiongea wakati wa wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars kwa viongozi wa mikoa iliyofanyika leo (Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam. Katikati Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akifatiwa na Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi.
Viongozi soka kutoka katika mikoa inayoshiriki michuano ya Airtel wakifatilia Seminar elekezi ya Michuano ya Airtel Rising Stars iliyofanyika iliyofanyika leo (Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam. Mikoa inayoshiriki katika michuano ya mwaka huu ni pamoja na ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala and Morogoro kwa upande wa wasichana huku mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Mbeya, Mwanza and Arusha ikiwa ni kwa upande wa wasichana.
Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Semina elekezi ya michuano ya Airtel Rising Stars iliyoshirikisha wasimamizi na viongozi wa mikoa itakayoshiriki katika michuano ya Airtel Rsing Stars inayotegemea kutimua vumbi 20 Julai. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando na kulia ni baadhi ya viongozi wa TFF.
Shirikisho la Soka nchini (TFF), limewasisitiza viongozi wa soka ngazi za mikoa kutambua kuwa lengo kuu la michuano ya Airtel Rising chini ya vijana wa miaka 17, ni kuibua vijana kwa manufaa ya Taifa kwa baadaye na sio kulelekeza nguvu zao katika kupata matokeo mazuri uwanjani kama ambavyo watu wengi hufikiri.
“Tumegundua kwamba baadhi ya viongozi wa soka mikoani wana fikra tofauti na lengo la michuano hii, wao huangalia zaidi kupata matokeo mazuri uwanjani kuliko kutafuta vijana wenye vipaji kama lilivyo lengo la michuano hii. Na hii ndio sababu kuu ya ongezeko la tatizo la watu kuleta vijana waliozidi umri uliolengwa katika program hii”, amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...