Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
IDARA ya Uhamiaji katika awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete imeingiza zaidi ya Sh.bilioni 474 kwa kipindi cha miaka 10 ambayo imetokana na maboresho mbalimbali katika idara hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamishina wa Fedha na Utawala,Piniel Mgonja amesema kuwa katika awamu ya nne uhamiaji imeweza kufanya kazi ya kisasa kutokana na mifumo pamoja na ujenzi wa Chuocha kuendeleza maafisa wa idara hiyo.
Amesema katika utoaji wa hati ya kusafiria kwa mwezi wanatoa hati 5000 tofauti na miaka 10 iliyopita ambapo walikuwa wakitoa hati 2500 ambayo ilikuwa ikitokana na kuchukua muda mrefu wa kuchapa kuliko ivyo sasa zinachapwa kwa kompyuta.
Mgonja amesema katika suala la uhamiaji bado changamoto kutokana na kuwa na uwazi katika mipaka ambapo walifanya uparesheni kuwakamata zaidi ya watu 74 000 kati ya hao watu zaidi 66000 waliondolewa nchini.
Amesema wamezidi kuimarisha katika udhibiti wa njia za mipaka ili nchi isiweze kugubikwa na wahamiaji haramu.
Amesema katika kipindi kijacho hati kusafiria kwa nchi za Afrika Mashariki itakuwa moja ya kimataifa ili kuondoa usumbufu kwa wateja wao kutafuta mara kwa mara kwa hati ya kusafiria kwa Afrika Mashariki
Makamishina wa Idara ya Uhamiaji wa kwanza kushoto kutoka mwanzo ,Msemaji wa Idara ya
Uhamiaji,Naibu Kamishina wa Idara ya Uhamiaji ,Abbas Irovya ,Naibu Kamishina
Mussa Lyamba,Mratibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji ,Petro Malima ,Mhasibu
Mkuu Karunde ,pamoja na Mkaguzi wa Idara hiyo, Kyando wakimsikiliza Kamishina
wa Fedha na Utawala ,Piniel Mgonja katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya
Idara ya Uhamiaji Kurasini,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watenadaji wa ngazi za juu wa Idara ya
Uhamiaji pamoja na waandishi
wakimsikiliza Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji,Piniel Mgonja katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Ingawa watu wengi hawafahamu lakini Immigration duniani sio taasisi yenye lengo la kuingiza mapato kana kwamba wanajisifu kwa kuingiza pesa nyingi. La hasha madhumuni ya Immigration ni kilinda mipaka na kutunza kumbukumbu za raia wa nchi yao, kuwahudumia raia wake walioko nje wenye mahitaji ya huduma zao na vile vile kudhibiti wageni.
ReplyDeleteKama wanatoza tozo kwa shughuli zao basi huwa ni kwa taratibu za kurudisha gharama zao katika kutoa huduma hizo na si vyema wao kuwa na taswira na malengo ya kutengeneza faida, pale ambapo faida inakuwa lengo basi hii uleta mgongano mkubwa wa jamii na pia huvurunja mwenendo wa unchumi wa nchi.
Vigezo vya kupima mafanikio ya Immigration ni hivi:
Asilimia ya Wananchi wenye vitambulisho vya uraia (NIDA iko chini ya Immigration)
Asilimia ngapi ya wageni wana vibali halali kukaa nchini
Muda wa kusubiri huduma - mfano wiki ngapi huchukua toka mtu apeleke maombi ya passport yaliyokamilika na kupatiwa passport
Idadi ya wananchi waliokuwa na passport
Idadi ya Maombi ya Huduma Kupokelewa na idadi ya Yaliyotatuliwa
Idadi ya Sehemu za huduma mfano Njia zote za mipakani zina immigration office? au nyingine hazina?