Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao maalum cha kamati kuu ya CCM katika ukumbi wa White House mjini Dodoma leo jioni.
Kikao hicho pamoja na Mambo mengine kitachagua wagombea watano ambao majina yao yatapelekwa katika Halmashauri kuu katika mchakato wa kumpata mgombea atakaye peperusha bendera ya CCM kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar ambaye pia ni Rais wa SMZ Dkt.Ali Mohamed Shein,Kulia ni Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Philip Mangula na Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Rais Mstaafu awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa,wakiongea kabla ya kuanza kwa kikao

 Baadhi ya wajumbe wa kikao maalum cha Kamati kuu ya CCM kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Makamu mwenyekiti Bara Mstaafu Ndugu Pius Msekwa, Rais Mstaafu Zanzibar Ndugu Amani Abeid Karume, Mawaziri Mkuu wastaafu Cleopa David Msuya na Salim Ahmed Salim. Picha na Freddy Maro



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2015

    Hadi raha kabisa, marais na waziri wakuu wastaafu wamekaa bukheri wa afya bila ya kubugudhiwa.

    Mwenyezi Mungu atujaalie tuendelee hivi hivi tulumbane kwa nguvu za hoja na sio hoja za nguvu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2015

    Hao ndio tegemeo letu katika mahamuzi ye kuteua tano bora na hatimaye kumpata nani anayetufaa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu.
    Pia ni tumaini letu kuwa hatapendekezwa mgombea mwenye madoa au aliyewahi kupata dosari za kuhusishwa na rushwa au ufisadi

    ReplyDelete
  3. Hivi mbona wastaafu wengine hawapo? Kama vile Komandoo wa Zanzibar, Sam Malecela na Jaji Warioba?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...