KAMPUNI ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, jana ilikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa vituo 10 vya kulea yatima ikiwa ni mwendelezo wa kusaidia makundi maalumu katika jamii.

Akikabidhi misaada hiyo katika ofisi zake zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Msama alisema misaada hiyo ni sehemu ya fedha za mauzo ya DVD za Tamasha la Pasaka la mwaka huu.

Msama alisema kupitia mauzo ya DVD za Tamasha hilo ambalo lilifanyika April 6 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, wameona ni vema kuwafariji watoto yatima.

“Msama Promotions kama kawaida yetu, tumekuwa tukiyakumbuka makundi maalum katika jamii kama yatima, walemavu na wajane, hivyo leo hii tumewasaidia vitu mbalimbali watoto,” alisema Msama.

Alisema kampuni yake imekuwa ikifanya hivyo sio tu kwa kutambua wajibu wake katika kusaidia jamii, pia kuguswa na mazingira ya watoto hao wanahitaji sapoti ya jamii nzima.

“Watoto hawa ni kama wengine wanaokula, kunywa na kusaza katika familia zao, hivyo wanahitaji kusaidiwa na jamii nzima
si jukumu la wenye vituo vya kuwalea tu,” alisisitiza Msama.

Vituo vilivyonufaika na msaada huo wa jana, ni Chakuama, Maunga Centre, Mwandaliwa, Malaika, Honoratha, Zaidia, Mujahidin, Arahman na Almadina cha Tandale.

Miongoni mwa vitu hivyo vilivyopokewa jana na viongozi wao, ni unga, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni na vingine vingi kwa kila kituo.

Msama alisema mwendelezo wa msaada wa kampuni yake utafanyika pia mikoani baada ya uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji wa injili, Bonny Mwaitege utakaofanyika Agosti 2.
                     
Alisema sehemu ya mapato ya uzinduzi huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Diambond Jubilee, jijini Dar es Salaam, yatanunua baiskeli 100 kwa ajili ya walemavu.

Aliitaja baadhi ya mikoa itakayokumbukwa safari hii ni Iringa, Morogoro, Tabora, Dodoma, Tabora, Pwani, Mwanza, Mbeya na Singida.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula mtoto Haid Edwin (5) wa kituo cha Yatima cha Honorata cha jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula watoto wa kituo cha Yatima cha Al Madina cha jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanahabari wakijadiliana jambo kwenye tukio hilo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...