
Mwanasiasa
Mkongwe nchini,Kingunge Ngombale Mwilu akisisitiza jambo mbele ya
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) mapema
leo,nyumbani kwake makumbusho,jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.
.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii .
Mwanasiasa
mkongwe nchini,Kingunge Ngombale Mwilu amesema kuwa wanachma wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) ,umefika wakati muafaka sasa wa kuungana pamoja na
kuzika tofauti zao zilikuwa zikijitokeza hapo awali badala yake wasimame
imara kukijenga chama chao.
Akizungumza
na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam,Kingunge amesema CCM
inatambulika kimataifa kutokana na historia yake,hivyo lazima kiwe imara
wakiwemo viongozi wake wakiwashirikisha na wanachama wao .
Amesema
katika uchaguzi wa kutafuta mgombea urais uliofanyika hivi karibuni
mkoani Dodoma ulikiuka haki za wagombea kutokana na wagombea kushindwa
kwenda katika Mkutano mkuu wa wanachama na kujieleza.
Kingunge
amesema ,kilichotokea Dodoma sio halali na sio haki lakini chama cha
CCM lazima kiendelee,alisem na kuongeza kuwa "tumepata mgombea John Magufuli yeye sio
aliyefinyanga na wajumbe wa mkutano mkuu,hivyo tumuunge mkono kwa pamoja
na kupata ushindi wa kishindo",alisema Kingunge.
"Wana CCM watafute umoja wa kushikamana na kuwa Lowassa ana nafasi ndani ya
CCM,hivyo tuunde mazingira ya kutumia nguvu zilizopo CCM katika kushinda kwa
ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu",amesema Kingunge.
Amesema yaliyotokea Dodoma lazima yazungumzwe ili watu waweze kutoa duku duku zao kwa kile ambacho kimeonekana katika chama na ni changamoto kubwa ambayo inapaswa kufanyiwa kazi.
Mwanasiasa Mkongwe nchini na Kada
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kingunge Ngombale Mwilu (kushoto)
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
,Kuhusu mkutano mkuu wa chama hicho uliofayika mjini Dodoma hivi karibuni na
mchakato wa kumpata mgombea Urais na changamoto zilizojitokeza
Aibu ng'eeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteHata kama uchaguzi ulikiuka haki za wagombea kama anavyodai mzee Kingunge Ngombale Mwilu, kwani lengo lilikuwa ni nini? Si ni kumchagua mgombea ailiyekuwa imara zaidi kuliko wote? Kwani katika wote wale kuna mgombea ailiyekuwa imara zaidi kuliko Dkt. John Pombe Magufuli? Si ni ukweli usiopingika kwamba bila ya kufanyika vile angeweza kiurahisi kuchaguliwa mgombea mwingine ambae angekuwa ni mteremko kwa vyama vya upinzani wakati wa kupiga kura ya uchaguzi wa urais na hatimae kuwepo uwezekano mkubwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kushindwa? Waliyotumia njia ile ya kumchagua Dkt. John Pombe Magufuli ambae ndiye imara zaidi kuliko wagombea wengine wote waliona mbali kwa sababu siyo tu yawezekana sana Chama cha Mapinduzi (CCM) kikaendelea kuiongoza nchi yetu endapo Dkt. John Pombe Magufuli atashinda urais bali pia nchi yetu itakuwa imepata kiongozi mchapakazi, asiyekuwa na kashfa na atakaepiga vita ufisadi. Kwa ukongwe wa mzee Kingunge Ngombale Mwilu katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na uongozi wa nchi yetu, sikutegemea kabisa kama angeweza kukosoa hadharani mchakato wa namna alivyochaguliwa Dkt. John Pombe Magufuli kwani kwa kufanya kwake hivyo anatoa siri za Chama cha Mapinduzi (CCM) kitu ambacho hakikubaliki na anakwenda kinyume na kauli mbio ya chama chake isemayo "Umoja ni Ushindi". Narudia kusema hata kama uchaguzi ulikiuka haki za wagombea, lakini kwa kuwa aliyechaguliwa ni Dkt. John Pombe Magufuli hicho kwa kweli ni KITENDO KITAKATIFU kutokana na uimara mkubwa wa huyo aliyechaguliwa na maslahi mapana ya Taifa letu na wananchi wetu wote kwa ujumla. Wengi wetu tumefurahi kwa kuchaguliwa Dkt. John Pombe Magufuli kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na tutafurahi zaidi atakaposhinda urais na kuliongoza Taifa letu kama anavyotufurahisha katika kila Wizara anayopewa kuiongoza. Mungu ambariki Rais wetu Mtarajiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
ReplyDeleteHuyo mzee hana jipya mimi binafsi sikutegemea mzee kama huyo kwenda kusimama majukwaani hii leo badala ya kuwa mshauri tu.anatia aibu.
ReplyDeleteanaacha kupumzika kwa amani leo anasimama majukwaani.walicho dhamilia kimeshindikana.
Asitake kutuaminisha watz kwamba mtu wao alikua anakubarika kihivyo.Tena bila hata soni eti watanzania wanamhitaji wepi!? mimi binafsi sijawahi kumuhitaji so wasituongelee.
MZEE KAPUMZIKE HATA NYERERE AKIFUFUKA LEO AKUKUTE JUKWAANI ATAKUSHANGAA SAAAANA!
Traitor to the country and the party. GO AWAY Kinguge. Big disappointment.
ReplyDelete