Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho,Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa leo katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akizungumza na mamia wakati wa kutangaza adhima yake ya kujiunga na Chadema katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa (mwenye umvi) akiwa na viongozi wa UKAWA katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimpa kadi ya uanachama Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Regina Lowassa leo katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimpa kadi ya uanachama Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Regina Lowassa leo katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Mh.Lowassa akiingia kwenye Hoteli Bahari Beach kwa ajili ya kutangaza adhima yake ya kujiunga na UKAWA. Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa ametangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Katiba (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .
.
Mh.Edward Lowassa akiwa katika hadhara ya mamia kujibu maswali katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
.
Mh.Edward Lowassa akiwa katika hadhara ya mamia kujibu maswali katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli akiingia kwenye ukumbi wa mikutano ndani ya hotel ya Bahari Beach jijini Dar,kwenye mkutano wa Wanahabari jioni ya leo.
Mh.Lowassa akiwa na viongozi wa UKAWA katika Hoteli ya Bahari Beach Hoteli jijini Dar es Salaam jioni ya leo mara baada ya kutangaza rasmi azma yake ya kujiunga na ukawa.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam jioni hii alipokuwa akitangaza azma yake ya kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA.
Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Kadi yetu vp turudishie plz plz
ReplyDeleteumejimaliza mheshimiwa muulize ndugu yako mrema
DeleteJamani huyu lowasa sijui amekula maharage ya wapi huyuuu!!!
ReplyDeleteMZEE WANGU LAKINI USICHEZE NA AKILI ZA WATANZANIA UNATUFANYA SISI NI MAPUNGUANI . JUZI TU UMESEMA HIVI LEO UMEBADILIKA KAMA KINYONGA KHAAAA!
ReplyDeleteLowassa: "Siwezi kuhama CCM, ambaye anaona hafai ahame yeye"
Mbowe: "Lowassa ni fisadi na yuko katika list of shame".
Slaa: "Hatupokei makapi ya CCM"
Leo hii they all have same mindset!?
Hahaha...Tanzania nchi yangu nakupenda sana, ila ukombozi wako bado sana!
"Politics is a dirty game leave it to us who knw how to play it" chinua achebe
Uchaguzi wa mwaka 2005 sikupiga kura nilikuwa nje ya nchi. Uchaguzi wa mwaka 2010 pia sikupiga kura nilikuwa nje ya nchi kimasomo, na wala sikuumia kutotumia nafasi yangu kupiga kura. Lakini uchaguzi wa mwaka huu 2015 niko nchini na mwanzoni sikuona umuhimu wa kupiga kura, lakini hili la leo litanifanya niende kupiga kura kwa kweli hawa watu wanatufanya sisi hatuna akili wala kumbukumbu. Sijui wametugeuza kuwa sie wa wagonjwa wa Alzehimer au watu tuliopotewa kumbu kumbu?
ReplyDeleteMaghufuli sina mapenzi na wewe kivile wala sidhani kama CCM wako wasafi kivile lakini angalau mko wakweli na mna msimamo sio hawa leo wanatuambia hiki kesho wanasema na kufanya kile, kura yangu umepata Maghufuli na nitawahamiza watu wa nyumbani kwangu wote wakupigie kura hizo October.
Haya sasa na huyo Mchungaji tuone baada ya October kama atajiua au kujinyonga kweli kwa sababu Lowasa hatapata urais.
kusema kweli, huyu jamaa lazima kuna kitu cha ajabu na kutisha anakitafuta katika Tanzania hii.......Hivyo basi, achilia mbali viongozi wa upinzani, bali hata nyinyi wanachama wa upinzani muwe makini naye sana! sina mengi lakini akili kichwani
ReplyDeleteSASA HUYO SLAA MBONA HAONEKANI HAPO AU KISHA KIMBIA KUPISHA FISADI AUCHUKUE KITI?
ReplyDeleteWOTE NYIE CHADEMA HAMNAZO, HATA AIBU HAMANA KUMPOKEA MTU KAMA HUYO KINGIA KWENYE CHAMA CHENU TULIKUWA TUNA IMANI NA NYIE LAKINI NAONA HAMFAI TENA
Na mashati yetu ya kijani please
ReplyDeleteJamaa amechemsha sana, ulafi wa madaraka utamtokea puani.
ReplyDeleteHamno lolote, hii move aloifanya ndo itamtokomeza kabisaa kama ilivyotokea kwa Mrema. Uamuzi wa jazba huo. Pole Mr. Lowasa
ReplyDeleteKwisha habari yake huyo ni mroho tu wa madaraka
ReplyDeleteHakuna mtu mwenye uchu ya madaraka kama huyu jamaa na huu ndio mwisho wa ukawa na leo tumejua chadema ni chenye uchu ya madaraka ni chama hakifai hata kidogo kuongoza tanzania maana yake ndio mwisho wa jamuhuri ya watu wa tanzania I wapo ukawa wakichukua nchi wamekula matapishi yao wenyewe lowasa rudisha kadi ya ccm go to hell your not a polician power monger never never in lake zone big dad comando zulu
ReplyDeleteKweli mfa maji ahachi kuta tapa.
ReplyDeleteKadi yenu ilishatupwa jalalani maana ni aibu kuwa nayo.....Sasa mkafanye kitchen party number 2 za tatu bora au tano bora huko dodoma .
ReplyDeletekadi yenu iko sokoni wanafungia bizari.
ReplyDeleteuroho wa madaraka, hakuna kingine. Ila ushindwe katika jina la Yesu!
ReplyDeletekadi yenu itarudi, lakini mjue na sisi tunataka vitu vyetu mlivyohodhi!
ReplyDeleteleo mseomo wa wazee umetimia Wahenga walisema ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.kinachotokea kwenye medani za siasa ni ghiriba ulaghai na uzandiki kwa watz.mtu yule yule ambaye tuliaminishwa kuwa ni mwizi fisadi na amepata utajiri kwa njia za haramu leo tunaambiwa kuwa ni msafi na anafaa kuwa rais wa nchi hii.wakati fulani tuliambiwa kuwa alipokua waziri mkuu alishindwa kupeleka maji arumeru.na wakasema ataweza vp kupeleka akiwa rais maana huyu mtu awezi kuwa rais na hafai kuwa rais wa nchi kwa kua ni mwizi na fisadi na kama sio mwizi na fisadi aende mahakamani kumshtaki DK slaa aliyetoa kauli hy mpaka ss ajakwenda wala kukanusha kama yy sio fisadi.ss inakuje tena wale wale waliotuaminasha watz kuwa hy mtu ni fisadi na aende mahakamani na akwenda kushtaki leo tuamini vp kama mtu hy sio fisadi! watanzania wa leo sio wale wa mwalimu nyerere tumeshtuka watz.biashara mnafanya sio kwa ajili ya watz ni kwa ajili yenu na family zenu.lowassa sio mtu sahihi kwa watz wa leo ambao ukienda hospital kila kitu unalipia.lowassa hafai kuwa Rais wa nchi
ReplyDeletelowasa kuwa raisi never never tumegundua tumegundua sasa tunaeda weka kila kitu wazi lowasa hafai anataka madaraka kama kwa nguvu na hizo siasa za ukabila hatuzitaki kabisa na sasa ndio tunaanza lowasa he will never na chadema will never go to ikulu na plan zenu za ukabila na udini na hao viongozi wenu wa ukawa.
yusef
Tanzania tupiganie Katiba ya Wananchi, yenye nguvu kudhibiti Umimi katika Uongozi nyanja zote.
ReplyDeleteMbona kimy@@@@@???
ReplyDeleteAkikosa Urais 2015 ndio utakuwa mwisho wake wa maisha kwa jinsi anavyo usaka huo uongozi kwa udi na uvumba
ReplyDeletehakuna upinzani wa kweli Tanzania bali ni wa njaa na uchu wa madaraka. siyo muda mrefu chadema na upinzani mliimba nyimbo za ufisadi na 'list of shame' ambapo mlimtaja Lowassa kama kinara (papa) wa ufisadi, leo mmempokea kwa kishindo eti ufisadi ni muundo uliyopo ccm. jueni kwamba, kwa mtindo huo uongozi wa nchi hamtaupata ng'o hata kama CCM isipoiba kura. ilaa kama Mtanzania naamini kuwa mmefanya hivyo baada ya kuzuzuka na 10 biloni alizonazo Lowassa tayari kwa kampeni (zilipangwa kutunmika ndani ya CCm ila alibanwa kuzitumia) hivyo kulazimika kula matapishi yenu wenyewe (shame on you guys). bye bye Chadema na Ukawa Byebye Lowassa..... imekula kwenu...
ReplyDeletechadema, jibuni maswali haya
ReplyDelete1. la Baba wa Taifa juu ya wapi/namna Lowassa alivyopata mali zake.......
2. je ile 'list of shame' bado ipo???
3. je ule wimbo wa Lowassa kuwa kinara wa ufisadi bado upo??
LOWASA UMEJIMALIZA KWISHNEHI!!!! unapita nyayo za MREMA pole yako..uraisi utaishia kuusikia tu..bye bye
ReplyDeleteHaya ndio maamuzi magumu
ReplyDeleteMimi ni CDM DAMU, LAKINI HIKI KILICHOFANYWA NA MWENYEKITI WETU SIKIELEWI, AMEKIUZA CHAMA KWA FISADI, INAUMA SANA, CCM MNAKURA YANGU
ReplyDeleteWengi wanaoandika maoni hapa wafikiri politics ni kama lelemama
ReplyDeleteHuyu mheshimiwa hawezi kiuangusha CCM lakini nionavyo mimi anaweza kuleta pango kubwa,CCM ikae kitako na kufikiria njia za damage limitation siyo kupuuza tukio kama hili. He is the highest ranking cadre to leave the party, you can correct me if I am wrong.
Tumwombe Mungu atuvushe salaama kwani Mungu anamjua anayefaa kutuongoza kwa kipindi hiki.Kumbuka wale walio kuwa wametaka mwanamke mwenye dhambi apigwe mawe na jibu la Yesu.
ReplyDelete