Na Hassan Hamad, Milan, Italy 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewasili Mjini Milan nchini Italy kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya kiserikali. Katika uwanja wa ndege wa Milan, Maalim Seif amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Italy Dkt. James Msekela. 
Akiwa nchini Italy, Maalim Seif ambaye anamuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa yanayofanyika Mjini Milan, pamoja na mambo mengine atatembelea mabanda ya maonyesho ya Tanzania. 
Aidha anategemewa kufungua kongamano la bishara za Kitanzania litakalotanguliwa na burudani ya kikundi cha sanaa cha Bagamoyo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiongozana na balozi wa Tanzania nchini Italy Dkt. James Msekela, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Milan nchini Italy kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi nchini humo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa na balozi wa Tanzania nchini Italy Dkt. James Msekela, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Milan nchini Italy kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi nchini humo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, na balozi wa Tanzania nchini Italy Dkt. James Msekela, wakiwa pamoja na baadhi ya wajumbe wa ziara hiyo. (Picha na Salmin Said, OMKR, Milan)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...