Habari na picha 
na John Nditi
MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, Julai 6, 2015, amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Ulanga, ambapo moja ya jukumu kubwa lilikuwa ni kulihutubia baraza la madiwani wa halmashauri hiyo , ambalo lilikuwa na jukumu la kupitia majibu ya hoja za ukaguzi kwa mwaka 2013/2014.
Hata hivyo katika hotuba yake kwa madiwani hao kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo kupisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Mkuu huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuwapongeza madiwani na watendaji wa halmashauri kwa kuiwezesha kupata hati safi kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa huyo, hati safi hizo zilipatikana katika mwaka wa fedha wa 2010/2011. 2011/2012,2012/2013 na 2013/2014.
Mkuu huyo wa mkoa alisema , mafanikio hayo hawakutokea kwa kubahatisha ila yanatokana na kufanya kazi kwa ushirikiano, uadilifu na bidii, baina ya madiwani , watendaji wa halmashauri na wananchi wa wilaya ya Ulanga.
Hata hivyo aliwaambia madiwani hao na watendaji wa halmashauri hiyo , kuwa pamoja na mafanikio ya kupata hati safi , wasiridhike ama kutosheka na mafanikio na kuanza kubweteka.
“Lazima muendelee kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kudumisha na kulinda mafanikio hawa na kufikia kiwango cha juu kabisa cha mafanikio katika hesabu za halmashauri na kuendelea kupata hati safi isiyokuwa na msisitizo” alisema Mkuu wa mkoa.
Alisema , lengo ni kuifanya halmashauri hiyo kuwa ya mfano wa kuigwa na halmashauri nyingine za mkoa wa Morogoro na Tanzania nzima.
Hata hivyo alisema , kwa mwaka huo wa 2013/2014, halmashauri zote saba za mkoa pamoja na Ofisi ya Mkuu wa mkoa zimepata hati safi na kutaka kila halmashauri kufata misingi ya sheria za ukaguzi wa hesabu za serikali.

Mabaraza ya madiwani , kwa mujibu wa sheria na tangazo la serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi , anapaswa kuwa yamefikia ukomo wake kuanzia Julai 6 hadi 8, mwaka huu ili kupisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu. 
 Sehmu ya majengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.
 Madiwani wa Ulanga wakifurahia jambo wakati MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe akiwahutubia
MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe akiwahutubia madiwani wa Ulanga
MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, katika picha ya pamoja na madiwani wa Halmashauri ya Ulanga


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...