Usili wa kwanza wa Dance 100% (2015) umefanyika kwa mafanikio makubwa Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo makundi ya Team ya Shamba, The WT Group, WD, The Best Boys Kaka Zao na Team Makorokocho wameweza kushinda nafasi ya kuingia katika michuano kutoka wilaya ya Temeke.

Makundi haya yamechuana vikali na mengine 6 yanayokamilisha idadi ya makundi 11, UNI 6 Crew, GMF Crew, TWC, Dar Crew, Noma Sana Crew, na Viga Stars yaliyojitokeza kuwania nafasi hiyo katika usajili huo wa kwanza.

Mratibu wa mashindano hayo kutoka East Africa Television na East Africa Radio, Bi Happy Shame, amesema kuwa amefurahishwa na utulivu na amani ambayo wapenda burudani Temeke wameonyesha leo, huku pia kukiwa na vipaji mbalimbali kutoka makundi yaliyojitokeza katika usaili huo wa kwanza.

Akizungumza baada ya kumalizika michuano ya usaili huo, mratibu wa Dance 100% kutoka BASATA, Kwerugira Maregesi, mbali na kufurahishwa na vipaji vilivyojitokeza, amekumbushia umuhimu wa makundi hususan yale yanayotarajiwa kushiriki usajili unaofuata, kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa kujiwezesha kushinda, ikiwepo ubunifu katika mitindo ya kudansi, kuburudisha na muonekano, huku akishauri kupunguzwa kwa mitindo ya sarakasi na kuongezwa ladha katika upande wa dansi zaidi.

Majaji Super Nyamwela, Queen Darleen na Shetta wametumia umakini nkubwa kuhakikisha wanatoa alama zinazostahili kwa mujibu wa vigezo kwa washiriki wote, huku burudani mbalimbali zikijiri zikishereheshwa kikamilifu na watangazaji rasmi wa Dance 100 kwa mwaka huu, T-Bway 360 na mrembo Maggie Vampire.

Majaji pia kila mmoja kwa nafasi yake wametaka washiriki watakaoendelea kujitokeza kujipanga zaidi wakizingatia vigezo vilivyowekwa, ambavyo ndivyo wanavyovitumia kutoa maksi (alama) zitakazowawezesha kufikia ushindi.

Usajili wa pili wa mashindano haya makubwa kabisa ya kudansi utafanyika katika viwanja vya Don Bosco Upanga siku ya Jumamosi Tarehe 01 Agosti 2015, ambapo makundi mengine matano yatasakwa kushiriki katika michuano hiyo kwa mwaka huu.

Usikose kujionea kwa urefu yote yaliyojiri  pale TCC Chang'ombe katika mashindano ya usajili huo, kwa kutazama ting'a namba moja kwa vijana EATV, siku ya Jumamosi, kuanzia saa 12 na nusu jioni.

East Africa Television na East Africa Radio inaleta Dance 100% kwa kupewa nguvu na mtandao wa Vodacom Tanzania na Coca Cola ambao ndio kinywaji rasmi cha dance 100% (2015).
 Kutoka kushoto -Majaji wa mwaka huu kwenye Dance 100%  ni Super Nyamwela, Shetta na Queen Darleen wakiwa wanajumulisha matokeo ya washiriki kutoka Temeke.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...