Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu 

 Na Woinde Shizza,Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi mabaya ya ardhi yasiyozingatia mpango bora wa matumizi ya ardhi yamekua tishio kwa maeneo uhifadhi hivyo kupelekea uvamizi wa maeneo hayo na kutumiwa kwa shughuli za ufugaji na kilimo kinyume cha utaratibu.

Nyalandu amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa kati ya Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) uliofanyika jijini hapa,amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu utakaorithiwa na vizazi vijavyo mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi kuzingatiwa.

Waziri huyo amesema kuwa ujenzi wa miji katika maeneo ya uhifadhi ikiwemo Hoteli na kumbi za starehe unaathiri shughuli za uhifadhi hivyo amewataka wadau wa utalii kugawanya uwekekezaji kwa kuwekeza nje ya hifadhi.

“Mtu anayefikiria kujenga miji ndani ya hifadhi anakua hajapiga hesabu vizuri lazima tutawanye uwekezaji hoteli zijengwe nje ya hifadhi” Alisema Nyalandu.

Alisema kuwa kwa sasa Tanzania ina jumla ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) 21 ambazo ni kilometa za mraba 36237.7 na jumuiya nyingine 17 ziko katika hatua mbalimbali za uanzishwaji,amezitaka jumuiya hizo kuhakikisha kuwa zinawashirikisha wananchi katika kuhifadhi na kunufaika kwa mujibu wa sera ya wanayama pori ya mwaka 1998.

Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza watalii nchini Wilbard Chambulo alisema kuwa ili uhifadhi uweze kufanikiwa lazima wanakijiji wawe na hati miliki za maliasili ili waweze kuzitunza vyema. Chambulo anaeleza kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika uhifadhi ni nguzo muhimu sana kwa uhifadhi itakayosaidia kuwa na utalii endelevu kwa vizazi na vizazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...