MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Tanzania, Upendo Nkone amekuwa wa kwanza kujitokeza kusindikiza uzinduzi wa mwenzake Bonny Mwaitege, utakaofanyika Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,  Alex Msama Nkone amekuwa wa kwanza na ameonesha nia ya kumsindikiza Mwaitege kwa sababu ya ubora wa uzinduzi huo. “Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa yamefanywa kwa ustadi mkubwa  hasa hatua za mwisho za rekodi ya albamu hizo inayomaliziwa  jijini Mwanza na baadaye Nairobi,” alisema Msama.

Msama alisema Mwaitege anatarajia kuzindua albamu  tatu  ambazo zitashika anga la muziki huo hapa nchini kwa sababu ya ubora. Msama alisema sambamba na muimbaji huyo, mikoa mbalimbali imeonesha nia ya kutaka uzinduzi wa albamu hizo.

Aidha Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania kujiandaa kupata neno la Mungu kupitia muimbaji huyo.  Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako na njoo uombewe na Yesu yupo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...