Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Leticia Nyerere akinyanyua mikono ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuondoka katika chama hicho na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Viti Maalum
Chadema,Leticia Nyerere akifafanua jambo kwa waandishi habari juu ya kuondoka
katika chama hicho.

Waandishi
wa habari wakifuatilia kwa umakini maelezo ya Mbunge wa Viti Maalum
Chadema,Leticia Nyerere juu ya kuhama kwake katika chama hicho katika ukumbi wa
idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi
akiuliza swali kwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere ambaye
leo alikutana na waandishi habari juu kuhama chama hicho na kurejea CCM katika
mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo jijini Dar es
Salaam.
Na Chalila
Kibuda ,Globu ya Jamii.
MBUNGE wa Viti
Maalum wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mara ,Leticia
Nyerere amengatuka rasmi leo katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani
katika chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza
na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar
es Salaam,Leticia amesema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa
kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.
Amesema
mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo
kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.
“Moyo wangu umekuwa
ukisoneneka kutokana na kukaa Chadema na kuacha kukaa katika chama
kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa nasema narudi
nyumbani kutumikia”amesema Leticia.
Leticia
amesema kwenda Chadema alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu
dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM
kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa
akitoa katika michango ya bunge.
Amesema
wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM)hivyo katika
maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa
shahihi.
hakuwa na tija huko chadema, kwani we uncle ulimsikia bungeni hata siku moja? aongodke tu atuondolee kivuli huku chadema!!
ReplyDeletealikuwa hana tija huku chadema, kwani wewe ulimsikia akishiriki mjadala wowote huko bungeni> labda nililala kama wasirra!!
ReplyDeletealikuwa hana tija huku chadema, kwani wewe ulimsikia akishiriki mjadala wowote huko bungeni> labda nililala kama wasirra!!
ReplyDeleteTonge linasakwa kila kona
ReplyDelete