Meneja
Bidhaa wa benki ya Exim, Bw Aloyse Maro akiokota moja ya kura za wateja wakati
wa kuchezesha bahati nasibu ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya malengo
inayoendeshwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia
ni pamoja na mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini
Bw. Humudi Abdulhussein (kushoto) na mmoja wa
maafisa wa beki hiyo Bw George Musetti.
Benki
ya Exim Tanzania imeendesha droo yake ya
kwanza ya kampeni ya akaunti ya malengo inayolenga kuhamasisha utamaduni wa
kuweka akiba miongoni mwa watanzania.
Droo hiyo
iliyosimamiwa na Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini iliendeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita
jijini Dar es Salaam ikiwa ni
droo ya kwanza kati ya sita zinazotarajiwa kuendeshwa katika kampeni hiyo.
Akizungumza
mara tu baada ya droo hiyo, Meneja bidhaa wa benki hiyo, Bw. Aloyse Maro
alisema kampeni hiyo ilizinduliwa ikiwa ni sehemu ya jitahada za benki hiyo
kuwapatia wateja wake faida zaidi sambamba na huduma bora.
Alisema kwa
kuanzia, washindi waliopatakina kupitia droo hiyo walifanikiwa kujitwalia
zawadi za simu za kisasa aina ya iPhone 6 huku akitoa wito zaidi kwa wateja wa
benki hiyo kuwa na mwitikio zaidi kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo.
“Pamoja na
kutoa shukrani zetu kwa wateja wetu kutokana na mafanikio tunayoendelea
kuyapata ni vema pia tuwe mrejesho wa mafanikio haya kwao pia. Ni katika mazingira hayo ndio maana
tumekuwa na utaratibu wa kutoa zawadi kwa wateja wetu ili kufurahi nao
pamoja,’’ alisema Bw. Maro.
Zaidi
Bw. Maro aliwakumbusha wateja wa benki kuendelea kushiriki zaidi kwenye kampeni
hiyo kwa kuwa bado wananafasi zaidi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo
zawadi ya gari kwenye droo tano zilizosalia.
“Kampeni
hii inaendelea kwa kipindi cha miezi mitano na bado kuna zawadi zaidi kwa ajili
ya washiriki ikiwemo zawadi kuu ya gari ambayo itakabidhiwa kwa mshindi
mwishoni mwa kampeni hii. Hivyo tunaomba watu waendelee kushiriki zaidi,’’
alisema.
Sambamba
na zawadi hizo Bw. Maro aliongeza kuwa kampeni hiyo inatoa riba nzuri zaidi kwa
wateja wanaofungua akaunti hiyo ya malengo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...