Kama ambavyo aliweza kufanya vizuri
na singo yake ya kwanza, msanii Galaxy anatarajia kuchomoka na wimbo wake mpya
‘mzuri tu’ ukiwa umeandaliwa na Man Walter chini ya studio za Combination sound
hivi karibuni jijini Bongo.
The smart boy Galaxy Ikanda akiwa
maejipanga fresh kwa ujio wake mpya, alielezea sababu zinazompelekea kutumia
muda wake mwingi kujipanga na sio kukurupuka
“Muziki umekuwa na ushindani mkubwa sana kiasi inampelekea msanii
makini kuongeza umakini na ubunifu
kwenye utendaji Otherwise unaweza kujikuta kila siku umesimama sehemu moja
huendi mbele, kitu ambacho sikitarajii kulingana na jitihada nilizonazo”.
Alisema “kinachoturudisha nyuma wasanii wengi ambao tunachipukia ni kutokuwa na
nidhamu na kazi zetu wenyewa hata kwa wanaotusimamia (Managers), halikadhalika
tuna pupa ya kutafuta shortcut kuyafikia mafanikio kirahisi bila kufanya
juhudi, huku mi nasema ni kujidanganya”.
Galaxy ambaye kwa sasa yuko hewani na
wimbo unaojulikana kwa jina la ‘Tam Tam’ amewataka wasanii wenzake kuongeza
jitihata kwenye ubunifu na kuepuka kuzihusisha Sanaa zao na maisha yao binafsi
‘KUTENGENEZA KICKI’ kwa maana haiwasaidii na hii inachangia kuudidimiza muziki
wetu na Sanaa kwa ujumla.
“sioni sababu ya msanii kutengeneza
story ya uongo ili aweze kutoa wimbo wake, hii inaonesha dhahiri ni kutojiamini
na sijawahi kuona imemsaidia msanii kwa kufanya hivyo wimbo ukapata umaarufu
mwaka mzima, mara nyingi story za kutengeneza ili kutoa wimbo zikiisha na wimbo
umeisha so zinaua muziki wetu kama vipi tukaze” – Galaxy.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...