Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO),Tawi la Moshi Mjini wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na SABMiller East Africa, Roberto Jarrin alipokuwa akitoa mhadhara wa masuala ya biashara na masoko chuoni hapo, mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na SABMiller East Africa, Roberto Jarrin (kushoto) akibadilishana mawazo na Afisa Mipango wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO), Tawi la Moshi mjini, Wilfred Shangali mara baada ya kuhitimisha mhadhara wake wa masuala ya biashara na masoko kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu uliofanyika chuoni hapo juzi .
 Afisa Mipango wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO), Tawi la Moshi Mjini Wilfred Shangali akibadilishana mawazo na Meneja Mawasiliano na Mambo ya Nje wa TBL Emma Urio mara baada ya kumalizika kwa Mhadhara wa Biashara na Masoko uliotolewa chuoni hapo na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL na SABMiler East Africa Roberto Jarrin kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu.
  Meneja Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Urio akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kumalizika kwa Mhadhara wa biashara na masoko uliotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL na SABMiler East Africa Roberto Jarrin katika Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO), Tawi la Moshi mjini kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...