Akizungumzia
mchakato wa uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya
chama hicho, Mtemelwa alisema Julai mosi mwaka huu Chama Cha ACT-Wazalendo
kilifungua rasmi pazia la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali zikiweno
za Udiwani, Ubunge na Urais.
Alisema tangu kuanza kwa uchukuaji huo wa fomu
kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wanachama kuchukua fomu na hadi sasa kuna baadhi
ya majimbo na kata zina watia azma kuanzia wanne mpaka tisa jambo ambalo alidai
ni faraja kwa ACT Wazalendo.
"Kati ya majimbo 265 yakiwamo majimbo mapya
26 yaliyoongezwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ACT-Wazalendo
tumeshakuwa na waweka azma zaidi ya mmoja katika majimbo 226 kwa nchi nzima na
tunaamini mpaka kufikia mwisho wa uchukuaji fomu ndani ya Chama majimbo yote
265 yatakuwa yanawatia azma mbalimbali wanaosubiri kupitishwa na chama kwa
ajili ya uchaguzi mkuu," aliongeza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT
Wazalendo.
Alibainisha kuwa kichama mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa
nafasi ya udiwani ni julai 24, kwa nafasi ya Ubunge mwisho ni Julai 31 na kwa
nafasi ya Urais mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti Mosi, 2015.
"Kwa ngazi ya Taifa Halmashauri kuu itakutana Agosti 13 kwa ajili ya
kuteua jina la mgombea Urais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na
kupendekeza majina ya wagombea Urais kwenye mkutano mkuu,
Agosti 13, Mkutano
mkuu utamchagua mtu atakayepeperusha bendera ya Chama cha ACT Wazalendo katika
mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."
"Hivi karibuni
tumepokea taarifa kutoka katika miji ya Tarime na Rorya Mkoani Mara kuwa kuna
watu wanapita na kutangaza kuwa Chama chetu kimezuiwa kushiriki Uchaguzi kwa
muda wa miezi sita.
"Tumebaini lengo la upotoshaji huu ni kuwakatisha watanzania
tamaa juu ya ukuaji wa Chama Cha ACT-Wazalendo pamoja na dhamira yake nzuri ya
kuirudisha nchi katika misingi iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere.
"Tunawataarifu wananchi kuwa Chama chetu kitashiriki uchaguzi mkuu wa
Oktoba 25 mwaka huu kwa kuweka wagombea wa nafasi zote na Chama hakitakuwa
tayari kuona sehemu yoyote ya nchi mgombea wa CCM anapita bila kupingwa,"
alisisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...