Bendi maarufu ya muziki wa dansi Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, siku ya Jumapili 5 Julai 2015 ilitingisha jukwaa la Mamling Festival,liliofanyika kule Mining,Austria.
Kikosi kazi hicho  cha Ngoma Africa band kilipangiwa kupanda jukwaani saa 10 na dakika 30 alasiri,lakini maporomota walisogeza muda hadi saa 12 jioni ndio bendi hiyo ilipopanda jukwaani,
Muda ulisogezwa kutoka na hali ya jua na joto kali lililofikia nyuzi joto 38c,ambazo sio za kawaida kwa msimu summer barani ulaya.
Kikosi kazi kilipopanda jukwaani bila ya kuremba remba walianza kuporomosha muziki moto moto kama kawaida yao,kiasi cha kuwafanya waandaaji watoe mwaliko tena kwa bendi hiyo kushiriki onyesho la 2016 Mungu akijalia.
Ngoma Africa baada ya kumaliza kazi wamerudi katika maskani yao ya himaya Anunnaki,kule Ujerumani
 Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni wakitesa katika tamasha la  Mamling Festival, liliofanyika kule Mining,Austria.
 Ras Makinja akiongoza gwaride la Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, siku ya Jumapili 5 Julai 2015 katika tamasha la  Mamling Festival, liliofanyika kule Mining,Austria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2015

    ffu-ughaibuni aka ngoma africa band bin watoto wa mbwa Big up guys

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2015

    FFU wazee wa ubaya ubaya full gwaride NO kulala

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2015

    Ngoma Africa hongereni sana mnatisha mno, hard working guys

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2015

    WATOTO WA MBWA BWAKENI ! KILA ANAYEPITA MBELE NG'ATA TAFUNA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2015

    FFU naona maafande kazini atakayeleta fujo atakiona cha mtema kuni

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2015

    Kaka Kamanda ras makunja naona chini ya ulinzi wa kikosi hatumwi mtoto hapo oh peleka ujumbe kwa kamanda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...