NHC imeendelea kuwakagua vijana waliopewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali yatakayowezesha wananchi kujijengea nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri zote za Mikoa ya Katavi, Mbeya na kukamilika Mkoani Iringa. 

Kwa ujumla, vijana wana ari ya kutosha ingawa wana changamoto zinazohitaji msukumo wa Halmashauri zao, hasa za masoko ya matofali yao pamoja na mtaji wa kuwawezesha kuendelea na uzalishaji wa benki ya matofali ya kuuzia wananchi. 

Katika ziara ya NHC Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya hizo wameomba NHC isiwanyang’anye mashine na wameahidi kuwapa vijana mikopo na kuwasaidia malighafi za kuwawezesha kutengezea matofali hayo ikiwemo mchanga, sementi na udongo maalum kwa kazi hiyo. 

Hata hivyo, Mikoa ya Rukwa na Katavi muitikio wa vijana na Halmashauri hizo ukiacha Halmashauri ya Mlele ambayo inafanya vizuri, umekuwa hafifu sana na Shirika limelazimika kuzinyang’anya Halmashauri hizo mashine na kuzitaka kuomba upya kama bado wana azma ya kutumia mashine hizo kujiletea maendeleo ya kuwa na nyumba bora na kukuza ajira kwa vijana wao. Fuatilia yaliyojiri katika uhakiki huo katika picha.
New Picture (1)  
Kikundi cha ‘Mshikamano’ katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kikimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC BW. Muungano Saguya akiwaelezea namna ya kukuza ujuzi na kutumia Halmashauri zao kuongeza ufanisi wa kazi alipowatembelea nakusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili. Vijana hao wameshapewe eneo la muda la kuendesheea shughuli zao na wameanza kutengeneza tofali kwa ajili ya kuwauzia wanmanchi.
New Picture (2)
Hii ndiyo hali iliyojitokeza Mkoani Katavi katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda pale NHC ilipolazimika kuzitwaa mashine ilizotoa msaada kwa vijana ili waweze kujiajiri. Kikundi hiki cha Mpanda Hotel ni mojawapo ya vikundi vilivyonyang’anywa mashine Mkoani Katavi na Rukwa kwa Halmashauri sita za Mikoa hiyo ukiacha Mlele inayofanya vizuri, kushindwa kuzitumia mashine hizo ipasavyo. Halmashauri hizo zimetakiwa kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara baada ya kubainika kuwa vikundi vya awali vilundwa kisiiasa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...