Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaandaa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya watanzania waishiao nje ya Tanzania.  
Nchini Uingereza, Ubalozi unaratibu zoezi hilo kwa watanzania waishio Uingereza na Ireland. 

Tunaomba maombi hayo yaainishe Mkoa na Wilaya hitajika, aina ya matumizi ya ardhi hiyo kama ni Makazi, Biashara au Kilimo.

Maombi yawasilishwe kwa Viongozi wa Jumuiya za Watanzania katika miji/ maeneo wanayoishi, ambao watayaleta ubalozini kwa hatua zaidi. Au muombaji wanaweza kujaza fomu ya maombi kupitia tovuti ya Ubalozi kwa anuani ifuatayo: - http://tanzania-online.gov.uk/?page_id=309

Kwa maelezo zaidi piga simu namba: +44 207 569 1482 au tuma Barua pepe (Email): balozi@tanzania-online.gov.uk

*IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA, UINGEREZA*

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...