Vijana waliopata ushauri nasaha wa kuacha kutumia dawa za kulevya, wakishangilia baada ya Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguye (aliyevaa koti) kuwakabidhi msaada wa mashine tatu za kufyatulia matofali pamoja na mtaji wa sh. 500,000 katika hafla iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kigogo, Dar es Salaam jana.  Katikati mstari wa mbele ni Mchungaji wa kanisa hilo, Jackson Haranja ambaye pia ni mlezi wa vijana hao wapatao 40. Kulia mstari wa mbele ni Yahya Charahani ambaye ni Ofisa Mawasiliano wa NHC.
 Saguye akimkabidhi mashine hizo Mlezi wa vijana hao, Mchungaji Haranja
 Mchungaji Haranja akitoa shukurani kwa shirika hilo baada ya kupokea msaada huo ambapo aliseama utasaidia sana kuinua hali ya maisha ya vijana hao waliokuwa wameathirika na dawa za kulevya
Saguye akizungumza na vijana hao kuhusu lengo la kuwapatia msaada wa mashine hizo.
 (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2015

    Safi sana NHC kwa kuonyesha mfano

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...