Meneja
wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa
wilaya ya Singida, Alli Amanzi msaada wa mashuka 200 kwa ajili ya
hospital ya mkoa mjini hapa.(Picha na Nathaniel Limu).
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Alli Amanzi (kulia) akibadilishana mawazo na
Meneja Mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Singida, Agnes
Chaki (katikati) muda mfupi kabla Meneja NHIF hajakabidhi mashuka 200
kwa hospitali ya mkoa mjini hapa.Kushoto ni Afisa uthibiti ubora wa
huduma NHIF mkoani hapa, Dk.Edwin Mwangajilo.
Na Nathaniel Limu, Singida
HOSPTALI
ya mkoa wa Singida iliyopo mjini hapa,inakabiliwa na uhaba mkubwa wa
mashuka kitendo kinachochangia wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi
wakati wote wanapokuwa wamelazwa hospitalini hapo.
Hayo
yamesemwa na Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Henry Mgetta,
wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa mashuka 200
yaliyotolewa msaada kwa hospitali ya mkoa na mfuko wa taifa wa bima ya
afya (NHIF) mkoani Singida.Alisema hospitali hiyo yenye vitanda 300 vya
kulaza wagonjwa,inakabiliwa na uhaba wa mashuka 2,400 na magodoro 230.
“Hali
ni mbaya mno,shuka 100 tulizonazo,ni chakavu na kwa ujumla nazo hazifai
kwa matumizi ya binadamu.Wagonjwa wanaolazwa inawalazimu kutumia shuka
zao binafsi jambo ambalo halikubaliki”,alisema Dk.Mgetta. Alisema mbali
na uhaba wa shuka na magodoro,hosptali hiyopia ina uhaba wa vitanda na
hasa kwenye wodi ya wazazi, kitendo kinachochangia wajawazito wanne
watumie kitanda kimoja.
“Natoa
wito kwa wadau mbalimbali,waangalie uwezekano wa kuisaidia kwa hali na
mali hospitali yetu hii na vituo mbalimbali,ili viweze kutoa huduma bora
inayokidhi mahitaji ya wananchi”’alisema Dk.Mgetta. Kwa upande wake
Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki,alisema kuwa wametoa msaada
huo wa mashuka hayo baada ya kuombwa na serikali ya wilaya ya Singida.
Alisema
majukumu ya NHIF,ni pamoja na kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za
afya zinajitosheleza kwa kuwa na mahitaji yote muhimu kwa kutoa misaada
na vile vile mikopo ya kununulia dawa,vifaa tiba na uboreshaji wa
majengo.
“Nina
imani kituo cho chote cha afya,zahanati na hospitali,kinapokuwa na
vitanda,mashuka na mambo mengine muhimu kwa wagonjwa wanaolazwa,kitendo
hicho kitakuwa kinawajengea mazingira mazuri ya kuendelea na matibabu
bila usumbufu wo wote”,alifafanua meneja huyo.
Chaki
alisema NHIF itaendelea kutoa misaada mbalimbali kadri uwezo
utakavyoruhusu kwa lengo la kusaidiana na serikali katika kuboresha
utoaji wa huduma za afya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...