Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
VIONGOZI nchini wametakiwa kushiriki katika mkutano wa
mabadiliko ya tabia ya nchi utakaofanyika Julai 13 na 16 Addis Ababa Ethiopia.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mratibu wa Mtandao wa
Mabadiliko ya Tabia ya Nchi (CAN),Sixsbaty Mwanga amesema mkutano huo ni muhimu
kutokana hali iliyopo sasa katika mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuongezeka
ukame ,njaa pamoja na mafuriko, hivyo viongozi wanaweza kushawishi mkutano
katika kuongeza bajeti katika eneo hilo katika kukabiliana na majanga hayo.
Amesema
fedha ya kuweza kupambana na mabadiliko hazitoshi kufikia mwaka 2020, Tanzania
kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi itatumia Trilioni mbili kwa
mwaka kutokana na ambayo itakuwa imefikia katika mabadiliko ya tabia.
Mwanga
amesema fedha za mabadiliko ya tabia ya nchi zinatakiwa ziwekwe wazi ili
kusaidia wananchi kuweza kupata msaada pale panapotokea majanga ya ukame na
mafuriko na waketi mwingine fedha hizo zinapotea na kushindwa kutatua matatizo
yanayotokana na mabadiliko hayo .
Amesema
mikutano iliyopita haikuwa na changamoto ya tabia ya nchi lakini sasa tatizo
limezidi kukua kutokana na hali iliyopo kufikia mwaka 2020 vifo vitakuwa vya
kila siku vinavyotokana na mabadiliko hayo.
Amesema
katika malengo 17 ya maendeleo endelevu ya masuala ya tabia ya nchi yanatakiwa
kuangaliwa kwa katibu katika kila kpengele katika kuweza kukabili hali hiyo.
Hata
hivyo CAN inatarajia kufanya maandamano ya
matembezi amani Julai 12 ambayo itashirikisha zaidi ya wadau 400 wa
mazingira kushiriki na kupaza sauti, na matembezi hayo yataanzia katika chuo
Kikuu cha Ardhi (ARU) na kuishia katika kiwanja cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia ya NCH I(CAN) ,Sixsbaty Mwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano wa mabdiliko tabia nchi katika kuelekea mkutano wa viongozi utaofanyika nchini Addis Ababa,Ethiopia uliofanyika leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wakifatilia taarifa Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia ya NCHI(CAN) ,Sixsbaty Mwanga hayupo pichani katika mkutano uliofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...