Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kozi ya Tatu ya Chuo Cha Ulinzi wa Taifa (National Defence College NDC) huko Kunduchi jijini Dar es Salaam leo.Aliyeketi Pembeni ya Rais kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange na aliyeketi pembeni ya Rais Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na medali ya dhahabu ya mwanafunzi bora katika kozi ya tatu ya National Defence College(NDC) Brigedia Jenerali Aloyce Damian Mwanjile wakati wa mahafali iliyofanyika chuoni huko Kunduchi jijjini Dar es Salaam leo.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange baada ya kutunuku vyeti na zawadi kwenye mahafali ya kozi ya tatu ya National Defence College iliyofanyika Kunduchi jijini Dar es Salaam leo ambapo jumla ya wanafunzi 42 walihitimu masomo yao.(picha na Freddy Maro).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...